Home Biashara WAVUVI WALISHUKURU SHIRIKA LA MWAMBAO COASTAL COMMUNITY NETWORK TANZANIA KWA KUWAPATIA ELIMU...

WAVUVI WALISHUKURU SHIRIKA LA MWAMBAO COASTAL COMMUNITY NETWORK TANZANIA KWA KUWAPATIA ELIMU YA UFUNGAJI MIAMBA.

NA BONIFACE GIDEON, MKINGA

WAVUVI wa Samaki aina ya Pweza kata ya Boma Wilayani Mkinga Mkoani Tanga wapo kwenye furaha kubwa Baada ya Jana Oktoba 12 kuvua Pweza Wengi waliozidi Kg.800 ikiwa ni Historia kwenye maisha yao ya Uvuvi ambapo Walifanikiwa kuvua Samaki wakubwa wenye uzito wa Hadi Kg 5 na wa chini alikuwa na Gramu 500.

Kwa Mujibu wa Ismail Kassim Mwenyekiti wa Wavuvi hao Alisema Matokeo hayo makubwa Yanakuja ikiwa Baada ya kupatiwa Elimu ya kufunga miamba kwa Siku 90 ili Samaki aina ya Pweza wapate fursa za kuzariana na kukua na Baada ya hapo Samaki hao hukua Hadi kufikia uzito wa Kg 5-6 kwa Pweza mmoja,

“Tunashukuru Sana kwa kupatiwa Elimu hii ya kufunga Miamba Baharini ambapo Leo hii imeleta neema kubwa, Mvuvi mmoja Leo hii amerudi na Kg 39,35 kitu ambacho sio Cha kawaida kwani Awali mvuvi mmoja alikuwa anavua na pweza wa Gramu 200-700 , tunaomba Serikali itusaidie Vifaa kama Boti kwaajili ya kufanyia Doria Baharini hasa nyakati za Usiku ili tuilinde miamba yetu Mana Kuna Wavuvi wanafanya uharibifu nyakati za Usiku” Alisisitiza Kassim

Kwa Mujibu wa Wataalamu wa Pweza kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania linalojihusisha na Utoaji wa Elimu ya utunzaji Rasirimali Bahari kwa Jamii ziishizo ukanda wa Pwani inaelezwa kuwa ili pweza hukua kwa Siku 90 na Hana Uwezo wa kuhama zaidi ya eneo alilozaliwa ambapo huishi kwenye miamba Bahari na huhitaji utulivu mkubwa ili upate kukua kwa haraka.

Jumanne Sobo Msimamizi wa Mradi huo wa Uwezeshaji na Utoaji wa Elimu ya utunzaji Rasirimali Bahari kwa Wananchi waishio Mwambao wa Pwani aliwaambia Waandishi wa Habari wakati wa Hafla ya kufunguliwa kwa miamba hiyo kuwa haikuwa kazi Rahisi kufanikiwa kutoa Elimu hiyo ya ufungaji wa miamba Baharini kutokana na Mazoea ya Wavuvi ambapo kila mmoja alikuwa anajivulia kiholela,

“Awali kabla ya hatujawapatia Elimu mvuvi alikuwa anapata Pweza mwenye Gramu 200 japo Pweza wa kiwango Cha Gramu 200 ni kosa kisheria Wakati mwengine Gramu 500 na Hadi 700 kwa Siku Inategemea na Siku husika lakini kwasasa mvuvi kupata Pweza wenye uzito wa Kg 2-5 ni jambo kawaida Sana” Alisisitiza Sobo

Nae Msimamizi wa mauzo wa kiwanda Cha kusindika Pweza cha Alphakrest Ltd Cha Jijini Tanga Siraji Juma Alisema mahitaji ya Kiwanda hicho kwa Siku ni Tani 5-6 lakini kwasasa wanapata Tani Chini ya Wastani Watani 2 kwa Siku,

” Sisi kiwanda chetu kinamahitaji makubwa Sana ya pweza ambapo kwa Siku moja tunahitaji Tani 5 Hadi 6 lakini tubapata chini ya Tani 2 kwa Siku, Na kwa Siku kama ya Leo ya Ufunguzi wa miamba Baharini tutapata mzigo mkubwa angalau utasaidia kuzungusha Soko letu ” Alisisitiza Juma

Kwa upande wa Bei Alisema Wananua Hadi sh.8000 kwa Kg 1 na Baada ya makato ya Kodi mvuvi hupata Sh.6000,

“Hapa Bei zinapanda na kushuka lakini Richa ya hivyo Bado tunanunua kwa sh.8000 lakini tunatarajia Bei itapanda zaidi ya hapa huko mbeleni , hii inatokana na mahitaji ya pweza kuzidi kuongezeka kila Siku” Alisema Juma.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!