Home Kitaifa WAVUVI MUSOMA VIJIJINI WATAKIWA KUJITAYARISHA NA MIKOPO YA VIFAA VYA UVUVI KUJIINUA...

WAVUVI MUSOMA VIJIJINI WATAKIWA KUJITAYARISHA NA MIKOPO YA VIFAA VYA UVUVI KUJIINUA KIUCHUMI

Na Shomari Binda

WAVUVI katika jimbo la Musoma vijijini wametakiwa kujitayarisha na mikopo ya vifaa vya uvuvi vinavyotolewa na serikali ili kujikwamua kiuchumi.

Matayarisho hayo ni pamoja na kuunda vikundi na kutengeneza katiba kupitia maafisa uvuvi kwenye halmashauri na wataalam wa maendeleo ya jamii wa maandiko ya miradi.

Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo alipozungimza kwa simu kutoka bungeni na Mzawa Blog.

Amesema bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilipitishwa jana kinachofuata ni utekelezaji wake.

Muhongo amesema kama ilivyokuwa kwa mikopo ya awali ya zana za kisasa za uvuvi mikopo mingine ya riba nafuu inakuja na kuwataka wavuvi kujitayarisha.

Amesema bajeti ya mwaka 2024/2025 inayoanza kutekelezwa tarehe 01.07.2024 inatoa fursa kubwa kwa wavuvi kuboresha uvuvi wao na kujiinua kiuchumi.

Mbunge huyo amesema boti 450 zitakopeshwa pamoja na vizimba 497 vya kufugia samaki.

Amedai kuwa wavuvi wa jimbo la Musoma Vijijini wameanza vizuri kwa kupokea mikopo nafuu ya boti 5 na vuzimba 16 na kusema ni wakati wa kuongeza idadi ya zana hizo kwenye uvuvi

Ameongeza kuwa wanaostahili kutuma maombi ni vikundi mbalimbali vinavyotambuliwa na halmashauri vikiwemo vyama vya ushirika na kuwataka wengine kuunda vikundi hivyo zikiwemo kampuni za watu binafsi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!