Home Kitaifa WAVUVI KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI UKEREWE MKOANI MWANZA WAMEIOMBA SERIKALI KUIMARISHA HALI...

WAVUVI KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI UKEREWE MKOANI MWANZA WAMEIOMBA SERIKALI KUIMARISHA HALI YA USALAMA

Wavuvi katika Ziwa Victoria wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wameiomba serikali kuimarisha hali ya usalama ili kudhibiti ongezeko la vitendo vya uharamia kwenye ziwa hilo vinavyodaiwa kufanywa na maharamia kutoka ndani na nje ya nchi.

Wavuvi hao wakiwemo wa kisiwa cha ghana wamewasilisha kilio hicho kwa Mbunge wa Jimbo la ukerewe Joseph Mkundi ambaye amewahakikishia kuwa suala la uharamia kwenye ziwa victoria linatafutiwa ufumbuzi na wizara tatu za ulinzi,mambo ya ndani ya nchi pamoja na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki.

Aidha wakazi wa Visiwa vya Izinga na Zeru kata ya Ilangala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wameanza ujenzi wa shule ya msingi ili kuondoa adha ya watoto wao kusafiri umbali mrefu kusaka elimu.

Wakazi hao kwa kutumia nguvu zao wenyewe wamejenga boma lenye vyumba vitatu vya madarasa pamoja na ofisi moja ya walimu.

Serikali kupitia mfuko wa Jimbo la ukerewe imewaunga mkono wakazi wa visiwa hivyo kwa Kutoa shilingi millioni 12 zilizotumika kupaua chumba kimoja cha darasa pamoja na ofisi ya walimu.

Mkundi akiwa katika ziara ya kikazi kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe,wananchi wakaslalamikia ongezeko la vitendo vya uharamia katika ziwa Victoria.

Mbunge wa Jimbo hilo Mheshimiwa Joseph Mkundi awewahakikishia wananachi kuwasilisha malalamiko hayo serikalini ili hatua zichukuliwe na serikali katika kudhibiti vitendo vya uharamia kwenye ziwa Victoria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!