Home Kitaifa WAVUNAJI WA MAZAO YA MISITU WAVUNE NDANI YA MAENEO WALIYOPEWA VIBALI

WAVUNAJI WA MAZAO YA MISITU WAVUNE NDANI YA MAENEO WALIYOPEWA VIBALI

Na Scolastica Msewa, Bagamoyo
Wakala wa Huduma za misitu Tanzania TFS wamewataka Wavunaji wa mazao ya misitu nchini kuvuna mazao hayo ndani ya maeneo waliyopewa vibali ili taifa liwe na misitu endelevu na serikali iweze kupata mapato.

Akizungumza katika kikao cha Wadau wa mazao ya misitu Kanda ya Mashariki na Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro huko mjini Bagamoyo mkoani Pwani kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za misitu Tanzania TFS Prof. Dos Santos Silayo Kaimu Kamanda wa Kanda ya Mashariki PCO Mathew Ntilicha mvunaji anapopewa kibali cha kuvuna mazao ya misitu azingatie mipaka yake ya uvunaji sawa na kibali chake kinavyoelekeza.

“Tunapenda mnapopewa kibali cha uvunaji, mzingatie uvunaji wako usivuke eneo la uvunaji wako kwani usipovuna sawa na kibali chako malengo yaliyowekwa na serikali tunashindwa kuyafikia,” alisema.

“Sisi TFS tuna jukumu la kulinda rasilimali ya taifa katika misitu ikiwa ni pamoja na kukaa na wadau na kuwaelekeza na kusaidia sehemu enye changamoto ili malengo ya serikali yatimie” alisema.

Amesema TFS Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro huku Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambapo wameona ufanye kikao na wadau wa mazao ya misitu ili kukumbushana kanuni, sheria na taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu.

“Lengo la mkutano huu ni kujadili mustakabali wa kuendelea kuboresha kazi zinazofanywa kila siku TFS kwa jamii na serikali kwa ujumla” alisema Prof. Silayo.

Naye Mhifadhi Mkuu wa TFS, Yusuph Kajia amewataka Wafanyabiashara wa mazao ya misitu katika kanda hiyo, kufuata kanuni, sheria na taratibu za uvunaji na usafirishaji ili wafanye biashara iliyo halali.

“Nashauri wafanyabiashara ya mazao ya misitu kufuata kanuni na sheria ili waache kufanya biashara ya kubahatisha kwa kufanya biashara ya ujanja ujanja wakikamatwa watapigwa faini kubwa au kupoteza mzigo watapata hasara” amesema.

Mjasiriamali wa mkaa, Eva Kaaya amewataka wafanyabiashara wenzake kuwa waadilifu wa kulipia kama serikali inavyotaka. “Wajasiriamali wa mkaa tuwe waadilifu tulipie mazao yetu ya misitu,” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!