Home Kitaifa WAUMINI WA KIBOKO YA WACHAWI WAJITOKEZA HADHARANI

WAUMINI WA KIBOKO YA WACHAWI WAJITOKEZA HADHARANI

Na Magrethy Katengu–Dar es salaam

Siku kadhaa mara baada ya kufungwa Kanisa la Christian life(CLC) liloko Jijini Dar es salaam Temeke–Buza kwa Lulenge lililokuwa likiendeshwa na Raia wa Congo Dominique Dibwa aliyejikana kwa jina maarufu ” Kiboko ya wachawi baadhi ya waumini wake wamejitokeza hadharani kuomba serikali ikae naye mezani kuzungunza ili huduma irudishwe.

Akizungumza na Waandishi wa habari eneo ambalo lilikuwa likifanyika kutoa huduma ya ibada leo Julai 2, 2024 Nabii Komando Mashimo ameiomba serikali kama kuna mahali wanaona Kiboko ya wachawi alikosea katika utoaji wa huduama wangemwita na kumpa onyo.zaidi ya mara tatu kwa kiwa na yeye ni binadamu kuna kukosea angejirekebisha siyo kumfungia ghafla kwani huduma aliyokuwa akitoa ni ya kijamii kuhusu suala la watu kudai wanatozwa fedha hiyo ni mtu binafsi akihitaji huduma ya peke yake ndiyo aliweka utaratibu huo lakini haukutumia nguvu

Hata hivyo amesema huduma yeyote lazima iwe na changamoto makwazo na kwa sababu anayeiendesha ni binadamu mapungufu lazima yawepo hivyo kwa kuwa Serikali ni sikivu na inawapenda wananchi wake ni vyema utaratibu ungewekwa na kukutana meza moja ili huduma ifunguliwe

Naye Mchungaji Msaidizi wa Kiboko ya Wachawi Athanasi Christopher amesema yeye aliajiriwa kutoa huduma katika kanisa hilo tangu linaanza 2020 na walikuwa wachache vijana wengi wamenufaika wengine wanafanya usafi hivyo boda boda nao wafanyabiashara ambao wamefungua fremu za maduka sasa imewalazimu kufunga kwa kuwa hakuna wateja,

Aidha Jumapili ya tarehe 28,2024 Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni alisema kanisa hilo lina uwezo wa kukata rufaa na bado hajafikiwa na malalamiko hayo ofisini kwakwe limeishia ngazi ya chini husika inayoshughulika na Usajili w makanisa ,Asasi za kiraia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!