Home Afya WAUGUZI WASHAURIWA KUTATUA KERO ZAO ILI WAHUDUMIE VIZURI

WAUGUZI WASHAURIWA KUTATUA KERO ZAO ILI WAHUDUMIE VIZURI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka wauguzi nchini kutatua changamoto zinazowakabili Ili waweze kuboresha mazingira ya kazi wazifanyazo kuweza kutoa huduma bora za matibabu kwa watanzania.

Akizumgumza hivi karibuni Jijini Mwanza katika Mkutano wa 50 wa chama hicho Mkuu huyo wa Mkoa amesema wauguzi ni Nguzo Muhimu kwenye sekta ya afya licha ya kukabiliawa na mazingira magumu na hatarishi

Malima alisema kuwa wamefanya vizuri kuitisha mkutano huo kwani wataweza kupaza sauti Ili kasoro zilizopo zifanyiwe kazi na kila pande inayohusika.

Mmefanya Uamuzi wa Busara kuuleta Mkutano huo wa kitaifa Mkoani Mwanza niwasihi hakikisheni munakuja na mageuzi chanya Ili mufanye kazi katika mazingira bora na salama ” Alisema Malima

Amesema Serikali ya awamu ya sita imezidi kuimarisha sekta hiyo kwa kuhakikisha kunakuwepo na hospital na vituo vya afya vyenye ubora pamoja na upatikanaji wa dawa kwa wakati.

Dk Julius Shigella Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza alisema kuwa Mkutano huo utakuja na matokeo chanya kutokana na fursa za kuelimishana kupitia Tafiti za Kisayansi zilizofanyiwa majadiliano ya kutatua changamoto zinazoikabili.

Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya “wauguzi wetu mustakbari wetu” ulijumuisha washiriki 1200 wakiwemo wauguzi wakuu kuanzia ngazi mikoa na wilaya

Kwa Upande wake Rais wa Chama Cha wauguzi nchini Alexander Bayuya amesema Mkutano ulibeba mambo makuu matatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!