Home Kitaifa WATUMISHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA

WATUMISHI WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA

Na Mariam Muhando_Dar es salaam.

Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha Wafanyakazi Dkt Alice Kaijage amewatakata Watumishi Nchini kujitokeza katika Zoezi la Uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili waweze kuchagua Viongozi Bora.

Dkt Kaijage ameyabainisha hayo mara baada ya kufanya Ziara Leo Jijini Dar es salaam yenye lengo la Kusikiliza kero za Watumishi na kuzipatia Ufumbuzi sambamba na kuyaeleza mambo mema aliyoyafanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuleta Maendeleo hapa Nchini.

Amesema Nchi inaelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo Watumishi ni sehemu ya Taifa kwani Kila Mtanzania anaowajibu wa kupiga kura hivyo Rais Samia amewakumbuka katika kuwaletea maslahi Bora.

“Kwa mujibu wa Katiba yetu ibara ya tano inaelekeza ni wajibu wa Watumishi kupiga kura wasipo jitokeza katika zoezi hilo hawatoweza kupiga kura na kupata Viongozi Bora hivyo naawahidi yale yote mlioyapendekeza nitakwemda kuyafanyia kazi Kwa kuwa Serikali ya Rais Dr Samia Suluhu Hassani ni Sikivu na inakwenda kusimamia maslahi Bora ya Watumishi, “amesema Dkt Kaijage.

Wakati huo huo amewashukuru Viongozi mbalimbali wa wa Mkoa Dar es salaam Kwa mapokezi mazuri Mkoani humo.

“Namshukuru Mkuu wa Mkoa huu Katibu Tawala Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Meya wa Jiji na Mkurugenzi wa Jiji hili,” amesema Dkt Kaijage.

Mkuu wa Divisheni ya Rasilimali Watu na Utawala Selemani Kateti amempongeza Mbunge anaewakilisha Wafanyakazi Dkt Alice Kaijage kukutana na Watumishi mbalimbali hapa Nchini ili kusikiliza na kuzipatia Ufumbuzi changamoto zao.

“Hivyo namuahidi Mbunge Dkt Kaijage kuwa tutakwenda kuyafanyia kazi yale aliotuelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo maslahi ya Watumishi,”amesema Kateti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!