Home Kitaifa WATUMISHI WA NMB KAGERA WATOA MSAADA WA SETI 156 ZA MASHUKA HOSPTALI...

WATUMISHI WA NMB KAGERA WATOA MSAADA WA SETI 156 ZA MASHUKA HOSPTALI YA RUFAA YA MKOA KAGERA

Na Theophilida Felician Kagera.

Watumishi wa Benki ya NMB matawi ya Misenyi, Kayanga, Muleba, Kaitaba, Nkwenda na Kyerwa kwa umoja wao wameungana na kuchangia jumla ya seti 156 za mashuka na kuyatoa katika hosptali ya Mkoa Kagera.

Meneja wa tawi la NMB Wilaya ya Misenyi William Matatala kwa niaba ya wenzake wa matawi ya Muleba, Kaitaba, Kayanga, Nkwenda na Kyerwa akiwa katika hospatali hiyo hii leo Tarehe 7 February mwaka huu amesema kwamba watumishi hao wamewiwa kutoa msaada wa mashuka hayo kwa akina mama na watoto ili yaweze kuwasaidia wagonjwa wa makundi hayo wanapokuwa wamekuja kutibiwa katika hosptali hiyo.

Meneja huyo akisoma taarifa fupi baada ya kukabidhi mashuka hayo kwa mganga Mkuu wa hosptali hiyo katika word ya watoto amefafanua kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutoa vifaa nyanja mbalimbali hususani katika idara ya Afya na Elimu lengo ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali katika kuzipunguza changamoto za upungufu wa mahitaji kwa idara hizo.

“Sisi kama watumishi wa NMB matawi haya tumeguswa tukaona japo tufike katika hosptali yetu hii ya Mkoa make hosptali hii huwasaidia watu wengi wanaotoka wilayani na kuja kutibiwa hapa hivyo hichi kidogo tunaimani kitawagusa watu wote wawe wa hapa Bukoba mjini na wale wakutokea maeneo mengine ya wilaya za Mkoa huu kwa msaada huu moja kwa moja tunakuwa tumewagusa watu wa Karagwe, Kyerwa Muleba Misenyi Bukoba na maeneo mengine” Amesema Meneja Williamu Matatala.

Hata hivyo emeongeza kuwa Benki ya NMB na yenyewe imekuwa bega kwa bega katika kutoa misaada mara kadhaa maeneo mbalimbali pengine kutokana na maombi ya mahitaji kwa idara husika.

William ameushukuru na kuupongeza uongozi wa hospitali hiyo chini yake Mganga Mkuu kwa mapokezi mazuri waliyoyaonyesha kwao ambapo ameahidi kuendelea kuiishika mkono hosptali hiyo panapo Majaliwa.

Naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa hosptali hiyo Museleta Nyakiroto kwa niaba ya watumishi wenzake ametoa shukrani za dhati kwa Benki ya NMB hasa hasa watumishi wake hao waliojitoa na kuleta msaada wa mashuka hayo ambayo yatasaidia pakubwa katika kuboresha huduma zao kwa watoto na akina mama wanaokuwa wakiwauguza watoto wao “shuka ni muhimu sana katika utoajia wa huduma kwa wagonjwa wetu ukiwa na shuka za kutosha inakuwezesha kubaridisha shuka mara kwa mara na kwa mantiki hiyo inakupa muda wa kuzifanyia usafi na hivyo inasaidia kuepusha maambukizi kwa wagonjwa wetu hususani hii word ina watoto wa changa ambao wanahitaji kweli kuhudumiwa katika kiwango cha usafi wa hali ya juu sana naimani msaada huu utatusaidia mno ni washukuru tena wenzetu wa NMB bila shaka tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha huduma zetu katika hospatali yetu hii ya Bukoba Mkoa Kagera zinaboreka zaidi” Mganga Mfawidhi Museleta Nyakiroto akitoa msisitizo wa shukrani zake kwa NMB.

Naye Muuguzi Mkuu wa wa Mkoa Mercy Obadia Kagaruki pia naye ameshukuru kwa ujio wa Benki hiyo katika hopstali ya rufaa kwani msaada wa mashuka hayo ni mchango mkubwa utakaowezesha kuongeza huduma bora kwa watoto watakaopelekwa kutibiwa hospitalini hapo.

Baadhi ya akina mama waliowauguza watoto wao akiwemo Alinda Benjamini mkazi wa Rwamishenye Manispaa ya Bukoba wamewashukuru wafanya kazi hao wa Benki kwakutoa mashuka hayo kwa ajili yao pamoja na watoto watoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!