Home Kitaifa WATUMISHI MADINI WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA WAWEKEZAJI.

WATUMISHI MADINI WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA WAWEKEZAJI.

Wizara yatambua mchango wa watumishi waliostaafu na wanaotarajia kustaafu

Yamtambua na kumpongeza Mtumishi aliyeshinda Medali Tatu ( 3) Mashindano ya SHIMIWI

Asteria Muhozya na Tito Mselem- Morogoro

Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake wametakiwa kuweka mazingira wezeshi kwenye maeneo yao ya kazi yatakayovutia uwekezaji katika sekta ya Madini ili hatimaye Serikali iweze kunufaika na kupata mapato stahiki yanayotokana na rasilimali Madini.

Hayo yameleezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Adolf Nduguru kwa niaba ya Waziri wa Madini wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Morogoro na kutanguliwa na mkutano wa mafunzo kwa wajumbe wa baraza hilo.

Ameongeza kuwa, kwa kufanya hivyo kutaiwezesha sekta ya Madini kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa na kufikia mchango wa asilimia 10 ifikapo mwaka 2022 kama ilivyo ainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa .

Amesema kuwa, ili kufikia asilimia hiyo ni lazima wawepo wawekezaji na kwamba lengo hilo litafikiwa kikamilifu kwa watumishi kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kuhakikisha huduma wezeshi za kiuwekezaji zinatolewa, leseni zinatolewa, pamoja na mazingira mengine ambayo yatawezesha kutoa matokeo mazuri na hivyo kuchochea uwekezaji zaidi.

‘’Sheria ya Madini iko wazi, wawekezaji siyo wahisani, kama tunavyojua Serikali inapata mapato yake kupitia kodi na mirabaha. Aidha, kwenye uwekezaji mkubwa na wa kati kama serikali tuna hisa za asilimia 16 ambazo hazipungui thamani,’’ amesisitiza Katibu Nduguru.

Pia, amesema kuwa, kama watumishi wa umma, wanao wajibu wa kutekeleza majukumu yao na kusimamia sekta ya Madini kwa uzalendo, weledi, uaminifu na ufanisi ili kutimiza matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan ya kuona sekta ya Madini inalinufaisha taifa na watanzania kutokana na rasilimali ambazo nchi imejaaliwa kuwa nazo.

Ameongeza kuwa, kushiriki katika mkutano huo, kunatoa fursa ya kujitathmini na kupima mwenendo wa utekelezaji wa majukumu baada ya kutekeleza bajeti katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!