Na. Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM-TANZANIA
Jeshi la Polisi Nchini Kupitia Kitengo cha kuzuia na kupambana na Madawa ya kulevya (Anti Drug Unit)kwa kushirikiana na Polisi Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya Pamoja na vifaa mbalimbali.
Akitoa taarifa hiyo leo Mkuu wa Polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Nchini Kamishina msaidizi wa Polisi ACP AMON KAKWALE amesema kuwa kuwa kuanzia mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakani na kutolewa uamuzi.
Aidha amebainisha kuwa jumla watuhumiwa 377 walitiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na madawa ya kulevya.Pia amesema watuhumiwa 170 walifungwa vifungo mbalimbali kwa makosa hayo.
ACP Kakwale amekongeza kuwa vyombo vya moto vilivyo kamatwa na kutaifishwa ni Magari 8, Pikipiki 9, Boti 02 na Nyumba 01 vilitaifishwa na Mahakama kuwa Mali za Serikali.
Aidha Jeshi hilo halito muonea muhali mtu yeyote atakae kamatwa akijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na linawaomba wananchi kutoa taarifa za watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ili hatua zichukuliwe dhidi yao.