Home Kitaifa WATUHUMIWA 3 WAKUTWA NA PIKIPIKI 32 ZA WIZI

WATUHUMIWA 3 WAKUTWA NA PIKIPIKI 32 ZA WIZI

Na Magrethy Katengu J

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watuhumiwa 3 wakiwa na Pikipiki 32 walizoibiwa huku 13 zikitambuliwa na wamiliki wake.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 Kamanda wa Polis Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema Jeshi la polisi linaendelea na operesheni kali maalum ya kuzuia vitendo vya kihalifu na kukamata watuhumiwa mbalimbali wakiwemo wezi wa pikikipi zilizoibwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Operesheni hiyo ilianza tarehe 06 Februari 2024 na inaendelea mpaka sasa imemkamata Omari Mlopa (28) mkazi wa Mlandizi na wenzake wawili wakiwa na pikipiki 32 zilizoibwa na kuzifanya zao kujiingizia kipato kwa kuzikodisha kwa mikataba kwa watu mbalimbali na kujipatia pesa kila siku.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi Kanda maaluma ya Dar es Salaam na kubaini kuwa watuhuhumiwa hao walibadilisha namba za usajili za pikipiki hizo na kuweka namba bandia ili zisitambulike na wenyewe” amesema Kamanda

Naye Mmiliki aliyeibiwa Pikipiki Thobias Christopha amesema Pikipiki yake iliibiwa Aprili 17,2022 ambapo Dereva wake aliyemwajiri alikodiwa na abiria aliyevalia nguo za gwanda kumwomba ampeleke Mlimani City walipofika maeneo karibia na eneo hilo alimwambia asimamishe Pikipiki kisha akamwamrisha ashuke kwenye pikipiki wapita njia waliopomuuliza alisema alimwibia Simu Jana yake hivyo anampa adhabu ya kuruka kichurachura na baadae kumpora funguo na kutokomea kusikojulikana hivyo ameshukuru leo Pikipiki imepatikana ikiwa na hali mbaya lakini ameitambu

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linaendelea operesheni maalum ya ukamataji wa watu wanaokiuka sheria kwa kutenda makosa ya usalama barabarani hasa kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) na Bajaji.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2023 makosa ya pikipiki yaliyokamatwa ni 179,174, walioandikiwa faini za papo kwa hapo ni 178,937, waliofikishwa Mahakamani ni 237, waliohukumiwa adhabu ya kulipa faini 236, na mmoja alihukumiwa kifungo jela.

Kwa kipindi cha Januari hadi Februari 2024 makosa ya pikipiki yaliyokamatwa 36,775, walioandikiwa faini za papo kwa hapo ni 36,754, waliofikishwa mahakamani ni 14, na mashauri 7 yapo kwenye ofisi ya Mashitaka ya Taifa.

Katika Operesheni hii baadhi ya makosa ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara kwa waendesha pikipiki na bajaji ni kutovaa kofia ngumu, kupita taa nyekundu, ulevi, kuzidisha abiria, kupita barabara za mabasi yaendayo haraka pamoja na kupakia abiria kwenye taa za kuongozea magari.

Hata hivyo amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam licha ya kuendelea kutoa elimu juu ya uzuiaji wa makosa, ukamataji umelenga pia watu ambao wamekuwa wakikaidi na kutotii sheria kwa kuendesha vyombo vya moto bila kujali na baadae kujikuta wakisababisha ajali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!