Home Kitaifa WATUHUMIWA (27) MBARONI KWA MAKOSA YA KIHALIFU

WATUHUMIWA (27) MBARONI KWA MAKOSA YA KIHALIFU

Na Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watuhumiwa 27 kwa tuhuma za makosa ya kihalifu ikiwemo wizi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo TV Laptop, simu redio sabufa.

Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es salaam Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema Operesheni hiyo ilianza mwezi Novemba 2023 na linaendelea kusimamia mifumo ya kuzuia, kubaini na kupambana na vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali .

Operesheni kali maalum iliyoanza mwezi September, 2023 na inayo endelea katika maeneo mbalimbali jijini, imefanikiwa kuwanasa watuhumiwa mbalimbali wakiwemo watu wawili majina yamehifadhiwa kwa sababu za uchuguzi ambao wao huwatongoza wanawake, wanawawekea madawa ya kuwalewesha, kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji wa kingono na kuwapiga picha, kuwatishia kuwauua wakitoa siri za udhalilishaji huo na baadae kuwaibia simu, laptop na fedha” amesema Kamanda

Hata hivyo Watuhumiwa hao wamekamatwa na vitu mbalimbali walivyoiba ikiwa ni pamojana; laptop 10, simu za mkononi 305, za ainambalimbali, Televisheni 36, kamera 04, subwoofer 3, na Makava ya simu 160 Baadhi ya vitu vilivyokamatwa tayari
vimetambuliwa na wamiliki. Watuhumiwa Watashughulikiwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Sambamba na hayo watuhumiwa watatu wanashikiliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya Boti ambavyo ni engine mbili aina ya YAMAHA 200P betri mbili za Boti zenye thamani ya milioni Mia moja sitini laki tatu na elfu saba na Mia mbili (160,307,200) pamoja na gari namba T485 CWU aina ya Suzuki, mali TEUSIN VAN BAUREN mfanyabiashara raia wa Afrika Kusini. Watuhumiwa hao ni MSABAHA MICHAEL @ASKOFU miaka 37 mkazi wa Vikindu, JUMA ATHUMANI @DITO miaka 45 mkazi wa Mbagala, JOSEPH JANUARI miaka 23 dereva mkazi wa Tandale Kwatumbo.

Aidha Kamanda amesema uelekea sikukuu ya Chrismass na mwaka mpya Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherekea kwa amani na usalama umeimarishwa kwakiwango cha juu katika maeneo yote.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatakia wananchi wote maandalizi mema ya sikukuu za Chrismass na mwaka mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!