Home Kitaifa WATUHUMIWA 16 WA MAKOSA YA KUBAKA NA KULAWITI MKOA WA MARA WAPEWA...

WATUHUMIWA 16 WA MAKOSA YA KUBAKA NA KULAWITI MKOA WA MARA WAPEWA ADHABU

Na Shomari Binda-Musoma

JUMLA ya watuhumiwa 16 wa makosa mbalimbali ya ubakaji na kulawiti wametiwa hatiani kwa kupewa adhabu mbalimbali ikiwemo ya kifungo cha maisha jela, adhabu hizo zimetolewa kwenye Mahakama mbalimbali baada ya kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mara kufuatia ushirikiano wa wananchi.

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salim Morcase wakati akitoa taarifa ya operation maalum iliyofanywa na jeshi hilo mwezi mei katika kako chake na waandishi wa habari kilichofanyika Leo Mei 04, 2024 Ofisini kwake.

Amesema kwa upande wa makosa ya ukatili ya kijinsia ikiwemo ubakaji na kulawiti jumla ya kesi 36 zilifikishwa Mahakamani zikiwa na watuhumiwa 36 huku kati hizo kesi 13 zimepata mafanikio kwa watuhumiwa 16 kupewa adhabu.

Kamanda Morcase amesema mmoja wa aliyepewa adhabu ni Kilima Sunday mwenye umri wa miaka 22 aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 6 tukio lililotokea tarehe 15/7/2023 mtaa wa Kamnyonge manispaa ya Musoma.

Aidha amedai kuwa watuhumiwa wawili ambao ni Mulungu Mahela na Baraka Chacha wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika Mahakama ya Wilaya ya Butiama kwa kosa la kubaka.

Watuhumiwa wengine Marianya Marwa alikuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka katika Mahakama ya Wilaya Musoma na Twaha Iddy akihukumiwa pia miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti kwenye Mahakama ya watoto Musoma.

Kamanda huyo amesema katika adhabu hizo na nyingine zilizotolewa kwa watuhumiwa hao wa ubakaji na kulawiti kesi nyingine ambayo ilivuta hisia na huzuni ni ya mume kumpiga mke wake kisha kumlisha kinyesi chake tukio lililotokea novemba 22 mwaka 2023 Kijiji cha Sedeko wilayani Serengeti.

Katika tukio hilo mwanamke aitwaye Elizabeth John mwenye miaka 20 alishambuliwa kwa kupigwa maeneo mbalimbali kisha kulishwa kinyesi na mume wake aitwaye Nyaikorongo Mwita ambaye alikamatwa na kufikishwa Mahakamani kisha kupewa adhabu ya miezi 12 jela na fidia ya shilingi 2,000,000.

Vilevile Kamanda Morcase amesema katika operesheni yao waliyoifanya kwa lengo la kubaini na kuzuia uhalifu wamefanikikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 346. Kati ya hao watuhumiwa 07 wakiwa na jino la tembo.

Kamanda Morcase amesema jeshi la polisi pia limefanikiwa kukamata zana za uvuvi haramu ambazo ni nyavu aina ya timba pisi 54 pamoja na makoko pisi 6 ambazo zilikuwa zikitumika kwenye shughuli za uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria.

Hata hivyo amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kutoa taarifa pale wanapobaini au kutilia mashaka jambo lolote linaloweza kuhatarisha jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!