Home Kitaifa WATU WENYE UALBINO BADO WANAPITIA MADHARA MBALIMBALI.

WATU WENYE UALBINO BADO WANAPITIA MADHARA MBALIMBALI.

NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) Maiko Salali amesema watu wenye ualibino bado wanapitia madhira mbalimbali ikiwemo kuuawa na kukatwa viungo vyao.

Salali, amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili ambayo yalifanyika kimkoa katika jiji la Dodoma na kuratibiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Mkurugenzi huyo amesema licha ya uwepo wa juhudi mbalimbali za serikali na wadau bado siku za hivi karibuni kumeeendelea kuripitiwa matuko ya maauaji ya watu wenye ualibino pamoja na wengine kukatwa baadhi ya viongo vyao kutokana na imani za kishirikiana.

“Sisi kama Taasisi inayojihisisha na masula ya kulinda haki za watu wenye ulemavu mkoa wa Dodoma tumeadhimisha siku hii kwa kupeleka ujumbe kwenye jamii itambue uwepo watu wenye ulemavu na kuwapa fursa mbalimbali nakuwapa nafasi mbalimbali ili kuweza kujenga jamii jumuishi ambayo itakutanisha makundi yote.

“Kwahiyo sisi kama Taasisi tunaendelea kupeleka elimu kupitia mradi wetu ambao unaitwa chukua hatua paza sauti, zuia ukatili ambao tumekuwa tukiufanya chini ya ufadhili wa Women Trust Fund Tanzania, “amesema Salali

Naye, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma George Katabazi, amesema matukio ya ukatili wa kijinsia bado yapo hivyo ipo haja ya wadau pamoja na serikali kuendelea kushirikiana kukomesha hali hiyo.

“Suala la ukatili ni suala mtambuka hivyo ipo haja kwa kila mmoja wetu kushiriki katika kukomesha hali hiyo na sisi kama jeshi la polisi hatutamfumbia macho mtu yeyote atakaye bainika kufanya vitendo hivyo”amesema Kamanda Katabazi

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!