Home Kitaifa WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI PWANI.

WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI PWANI.

Watu watatu wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyohusisha lori na garindogo aina ya toyota alphard iliyotokea katika kijiji cha Mbwembwe wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa anayo taarifa ya tukio hilo na yupo njiani kuelekea eneo la tukio taarifa zaidi kuusu ajali hiyo atatoa hapo baadaye.

Nimesikia hivyo nipo njiani naelekea huko kwenye tukio,”- Kamanda Pius Lutumo.

Diwani wa kata ya Mbwewe Omary Msonde amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa kumi na mbili alfajiri ya leo Desemba 28, 2023 kwenye eneo hilo.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Albert Msando kupitia mitandao wa kijamii amesema kuwa waliofariki ni familia ya Diwani wa Kata ya Kabuku, Halmashauri ya Wilaya Handeni mkoani Tanga, Nurudin Semnangwa ambapo amepoteza mke, mtoto na dada wa kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!