Home Kitaifa WATU WANNE WANUSURIKA KUFA KWA MLIPUKO WA SIMU.

WATU WANNE WANUSURIKA KUFA KWA MLIPUKO WA SIMU.

Na Mwandishi Wetu

Watu wanne wamenusuriko kifo mara baada ya bajaji namba MC 567 CJK aina ya TVS iliyokuwa ikitoka maeneo ya stendi kuu ya mji wa Njombe kuelekea katikati ya mji kupinduka kutokana na mlipuko mkubwa wa simu ya abiria uliosababisha moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema bajaji hiyo imepinduka kutokana na dereva kugeuka nyuma kutokana na taharuki ya kulipuka kwa simu ndogo mali ya Siston Antony katika barabara kuu ya Njombe-Songea majira ya saa tano asubuhi.

Moto umelipuka mkubwa na dereva wa bajaji akageuka kuangalia abiria wake na kushindwa kuiongoza akaiachia bajaji wakapinduka”amesema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema baada ya ajali hiyo polisi imeweza kuingilia kati kutokana na mmiliki wa bajaji kutaka kulipwa na abiria mmiliki wa simu iliyosababisha mlipuko na kupelekea kupinduka kwa bajaji na kuharibika.

Aidha Kamanda Issa ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuwa na bima za vyombo vyao ili kuepusha usumbufu kama huo huku pia akitoa rai kwa wamiliki wa simu kuwa makini na matumizi ya simu zao,na kubainisha kuwa abiria wote waliweza kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya majeraha madogo na kuruhusiwa kutoka ili kuendelea na shughuli zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!