Home Kitaifa WATU WANNE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI BIHARAMULO

WATU WANNE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI BIHARAMULO

Na Theophilida Felician Kagera.

Watu wa nne wanashikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa tuhuma za kukutwa na Nyara za Serikali ambazo ni meno mawili ya Tembo moja likiwa na uzito wa kilogram (4.75) na lapili likiwa na uzito wa kilogram (4. 40) ngozi ya fisi, kishwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya Nyati, mkia mmoja wa Nyati, ngozi ya Swala pala pamoja na silaha mbili aina ya gobore pamoja na risasi tatu za kienyeji aina ya gololi ambazo hutumika kwa ajili ya kuua wanyamapori.

Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa watu hao mbele ya waandishi wa habari kamanda wa hifadhi hifadhi ya Ibanda na Kwerwa ACC Fredrick M. Mofulu katika eneo la makao makuu ya kituo cha Polisi Mkoa Kagera amesema kuwa mnamo Tarehe 13 February mwaka huu majira ya saa tatu usiku Jeshi la hifadhi za taifa Ibanda _ Kyerwa na Rumanyika _ Kagarwe walifanikiwa kukamata jangili wanne (4) wakiwa na Nyara hizo za Serikali katika Kijiji cha Muungano na Lusahunga wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Kamanda Fredrick ameeleza kuwa mafanikio ya kuwakamata watu hao yalitokana na kupata taarifa za kiintelejensia za uwepo wa mtandao wawatu wanaojihusisha na ujangili wawanyama pori pamoja na biashara ya Nyara za Serikali.

Hata hivyo amesema kwamba baada ya watu hao kukamatwa kikosi cha Askari wa Jeshi la uhifadhi wa wanyamapori na misitu (TANAPA) walishirikiana na Jeshi la Polisi wilaya ya Biharamulo katika kufanya hatua mbalimbali zikiwemo za upelelezi na ufunguaji wa majalada ya kesi.

Waliokamatwa ni Raphaeli Daudi Lugaira umri miaka( 44) Musukuma, Fikiri Simon Lugaira umri miaka (43) msukuma, Majaliwa Isaya Charles Umri miaka (42) Msumbwa, Warwa Budura Rupilya umri miaka (45) msukuma.

Kamanda Fredrick ametoa rai akisisitiza kuwa Jeshi la uhifadhi wa wanyamapori na misitu linawataka watanzania wote kutokujihusha na vitendo vya ujangili dhidi ya maliasilii kwani Jeshi hilo liko imara na kwayeyote atakayethubutu kushiriki vitendo vya ujangili atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwingineko Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera William Mwampaghale akiwa sambamba na kamanda huyo wahifadhi naye ameeleza kuwa wataendelea kushirikiana na wenzao wa hifadhi katika kufanya Oparesheni kabambe katika hifadhi zote za Mkoa huo lengo nikuhakikisha wale wote wanaojihusisha na ujangali wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria huku akiongeza kuwa watu hao wanne watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo wakabili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!