Na Magreth Mbinga
Taasisi inayoshughulika na kutoa mitaji kwa wawekezaji binafsi ya aecf imetenga Dola za Marekani Milioni 3.7 kwaajili ya kuwawezesha wajasiliamali binafsi kuweza kubuni na kuweza kusambaza teknolojia rahisi na zakisasa za kupikia katika maeneo ya vijijini .
Hayo yamezingumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Ferchesmi Mramba katika ufinguzi wa mkutano ambao umeandaliwa na eacf ambapo wameelekeza nguvu katika nishati ya kupikia hasa kwa maeneo ya vijijini.
“Teknolojia wanazolengwa kwa sasa ni LPG waweze kuipeleka vijijini ,makaa ya mawe ambayo yamechanganywa na vitu vingine kuweza kutumika kwaajili ya kupikia na kutengeneza majiko ya kisasa kama ni majiko ya makaa yaweze kutumia makaa kidogo au kama ya kuni yaweze kutumia kuni kidogo ” amesema Mramba.
Pia Bwana Mramba amesema wanakuja na teknolojia ya kisasa ambazo wanaenda nazo vijijini na Wizara ya nishati imeweka mkazo mkubwa sana katika eneo la teknolojia ya nishati ya kupikia .
Aidha Mkurugenzi wa AECF Victoria Sabula amesema mradi huo unataka kuokoa ukataji wa misitu na kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa tumeona tuwasaidie wawekezaji wadogo Tanzania.
“Hii itasaidia kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa 50% ya ya watu wa Dar es Salaam wanatumia mkaa tumekutana ili tuweze kutoa msaada kwa wawekezaji wadogo waweze kuwafikia wananchi wapike chakula safi bila kuchafua mazingira kwa kutumia nishati safi za kupikia” amesema Sabula.
Sanjari na hayo Meneja wa maradi wa Tanzania Clean Cook Program TCCP ambao umezinduliwa Fredrick Tunutu amesema mradi utafanya kazi na makampuni ya nishati ambayo yanasambaza nishati safi za kupikia mijini na vijijini ikiwa na lengo ni kutatua changamoto ambazo wanakutana nazo.
“Baadhi ya makampuni yanakutana na changamoto ya mtaji ,maswala mazima ya biashara na mengine yanachangamoto zinazotokana na miundombinu ya baadhi ya maeneo mradi huu utasaidia kuwaondolea wajisiriamali changamoto hizo kuweza kuwapatia kiasi cha pesa ili kuweza kuzitatua” amesema Tunutu.
Vilevile mradi huo unatarajia kuunga mkono makampuni kuanzia kuni hadi kuni na tano katika makampuni hayo wanategemea wataweza kusambaza nishati hizo kwa idadi ya elfu 60 iwe ni majiko sanifu au LPG .
“Kama watasambaza kwa idadi ya elfu 60 tunatarajia watafikia watu laki tatu ambao watafaidika tunategemea kwa miaka mitatu makampuni ambayo yatapewa huu mradi watasambaza teknolojia ya nishati safi elfu 60” amesema Tunutu.