Na Scolastica Msewa, Kigamboni.
Madrasat Hidaya Islamic Centre ya Kigamboni jijini Dar es salaam siku ya tarehe 7 mwezi huu inatarajia kuongoza waislamu na dini zingine nchini kufanya ibada maalumu ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Dakt. Hussein mwinyi na taifa kwa ujumla ili Mwenyezi Mungu aendelee kutupa heri, Upendo na mshikamano.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Dua maalumu ya kuombea taifa na Viongozi wa nchi Omary Kombe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Madrasat Hidaya Islamic Centre huko Kigamboni jijini Dar es salaam.
Amesema Dua hiyo maalumu itafanyika kwa lengo la kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ally Mwinyi na taifa Zima kwa ujumla ili mwenyezi Mungu aendelee kutupa kheri, Upendo, mshikamano na kuendelea kudumisha amani katika taifa na Dunia nzima.
Dua hiyo itafanyika tarehe 7 mwezi huu katika viwanja vya Mnadani darajani Kigamboni jijini Dar es salaam kwa kushirikisha vituo vya kulelea watoto yatima, viongozi wa dini, serikali, vyama vya Siasa na jamii kwa ujumla.
“Hivyo tunachukua fulsa hii kuwaalika watu wote kushiriki kwa pamoja ili kuliombea taifa letu kwani tunatambua Kazi kubwa na majukumu makubwa walio nayo Viongozi wetu katika kuliomgoza taifa letu la Tanzania”
“Sisi kama sehemu ya jamii tunaowajibu na Haki ya kuliombea taifa na Viongozi wake kwa mwenyezi Mungu ili azidi kutubariki kama taifa na kuwabariki Viongozi wetu katika kuliomgoza taifa”
“Tunaamini Dua hii itazidisha chachu ya kudumisha amani na Upendo katika jamii ambayo ndio msingi mkubwa wa nchi yetu”
Alisema “Rais Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi katika uongozi wao wamefanya kazi kubwa sana katika Kila sekta na hivyo tutazidi kuwaombea ili kazi iendelee kwa maslahi mapana ya taifa letu”
Aidha akizungumzia masuala ya ukatili wa kijinsia na ukosefu wa maadili katika jamii Omary amesema “Watanzania tudumishe Mila na destuli zetu ikiwa ni kuthibiti na kukabiliana na janga kubwa la ukatili wa kijinsia na ukosefu wa maadili katika taifa letu.
“Sio hekima Wala busara kufanya matendo au tabia ambazo zipo kinyume na maadili yetu hata vitabu vitukufu vya mwenyezi Mungu vinakataza matendo au tabia ambazo ni kinyume na maadili ya mwenyezi Mungu na jamii”
Amesema watoto, Wanawake ni waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia unaoendelea watu wanawatesa watoto na Wanawake ingawa kina baba nao wanafanyiwa ukatili ila wengi wao hawajitokezi hadharani kulalamika.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hidaya Islamic Centre ya Kigamboni jijini Dar es salaam Twahili Shaibu amesema Dua hiyo itahusisha Watanzania wote bila kujali tofauti za kidi kwani lengo ni kuombea Viongozi na taifa letu kwa ujumla.
Amesema Dua hiyo itaambatanisha na mahulidi ambapo pia aliwasisitiza Watanzania kuombea taifa hasa kutokana na taarifa za kuwepo kwa mvua za elinino ili zisilete madhara nchini.
+++++++++++++