MKUU wa Wilaya Biharamulo Kemilembe Lwota ameziagiza Mamlaka za serikali za kata na vijiji wilayani humo kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda shule na si vinginevyo.
Kemilembe ametoa maagizo hayo Julai 15,2022 wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Nyakanazi kata Lusahunga ambapo ameeleza kuwa kumekuwepo na tabia ya watoto kufanyishwa biashara hasa maeneo yenye mijini wilayani humo.
Ameeleza kuwa katika kuhakikisha kila mtoto wa Kitanznaia anapata elimu, serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia imedhamilia kutoa elimu Bure kuanzia darasa la awali hadi kidato Cha sita hivyo hakuna sababu ya watoto kuendelea kulandalanda mitaani.
“Tunaye Rais Mama anayejali watoto wake, ameamua watoto wote waende shule, mji huu wa Nyakanazi unakua kwa kasi sana lakini umekumbwa na wimbi la watoto kufanya biashara barabarani hili halikuabaliki.” Amesisitiza Kemilembe.
Katika Mkutano huo pia Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe Mhandisi Ezra John Chiwelesa amewataka wananchi kuendelea kuchapa Kazi ili kuweza kujikwamwamua kiuchumi huku akieleza mambo mbalimbali ambayo serikali imeyafanya katika wilaya ya Biharamulo.
Mhandisi Ezra amesema kuwa katika kutatua changamo ya Wananchi kuhusu maeneo ya kulima, tayari serikali ya mkoa wa Kagera imeanza kubainisha maeneo kutokana na maagizo ya Mhe. Rais Samia aliyoyatoa hivi Karibuni alipokuwa ziarani mkoani Kagera.
Chiwelesa amezitaka Mamlaka zinazohuaika kuhakikisha zinatenda haki wakati utakapofika wa kugawa mashamba hayo ili kila mwananchi aweze kupata na si kwa wale wenye pesa.