Home Kitaifa WATOTO TISA WAMEZALIWA KWENYE KAMBI ZA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

WATOTO TISA WAMEZALIWA KWENYE KAMBI ZA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

Watoto tisa wamezaliwa kwenye kambi za Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji wilayani Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumzia Maendeleo ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji mjini Kibaha baada ya kupokea Msaada wa nguo zenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 7 kutoka Umoja wa Wana Rufiji na Kilwa UMARUKI Mratibu wa Maafa mkoa wa Pwani Rose Kimaro amesema katika makambi ya kuhifadhi Waathirika wa mafuriko wa Kibiti na Rufiji wapo kina mama wamejifungua ambapo mpaka sasa watoto tisa wamezaliwa ikiwa mama mmoja alijifungua watoto mapacha katika Kambi ya Kibiti.

Rose ameshukuru timu ya uongozi wa UWT taifa ukiongozwa na Mama Mary Chatanda ambao walifika na kuleta misaada ya mavazi na mahitaji mbalimbali ya kusitili wale watoto ambapo tayari walipata vifaa mbalimbali kama baby show, pampas, kanga, na madela kwa kina mama hao waliojifungua.

“Tuliwagawia vifaa hivyo na kati ya watoto hao tisa kwa upande wa Wilaya ya Rufiji Watoto sita yaani wamama sita wamejifungua na Watoto watatu wamezaliwa wilaya ya Kibiti” alisema Rose.
Amesema wanashukuru kwa Wahisani mbalimbali, serikali kwa kuwasaidia misaada mbalimbali ambayo inawasaidia Waathirika wa mafuriko kwa Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mafia ambako kimbunga hidaya kilileta mafuriko na kuathiriwa miundombinu na makazi ya watu wilayani Mafia.
“Lakini pia wapo watoto chini ya miaka mitano hivyo tunashukuru mashirika ya Kimataifa na mashirika yasiyoya kiserikali na Wadau mbalimbali wakiwemo UNICEF wamefika kutusaidia vifaa mbalimbali kwaajili ya kina mama kufua, kujistili kama vyombo vya jikoni”

“Pia Ofisi ya Waziri Mkuu tunashukuru kwa kuleta maturubai yameweza kutusaidia kwaajili ya kuwatenga akinamama wenye watoto, watu wazima wa umri tofauti” alisema Rose.

“UNICEF walituletea mahema makubwa na vifaa vya michezo vya kusaidia watoto chini ya umri wa miaka mitano wanatakiwa kwenda shule ambao tangu watolewe kwenye maji ni zaidi ya mwezi Sasa walikuwa hawana vifaa vya michezo na hawakuwa na sehemu kwaajili ya kusoma”

“Yale mahema yamesaidia wanapata elimu pale wapo Walimu wanajitolea wanawafundisha katika Wilaya za Kibiti na Rufiji hivyo tunashukuru sana kwa kutukimbilia kutuletea misaada”

Akizungumzia hali ilivyo kwa Sasa Mratibu huyo wa Maafa mkoa wa Pwani amesema mvua zimepungua na maji yanaendelea kupungua na baada ya kutoa ushauri nasaha baadhi ya Waathirika wamekubali kutoka kambini na kwenda kuungana na famila, ndugu na jamaa zao.

Amesema Waathirika 286 bado wapo kwenye kambi kati ya 498 waliokuwa kwenye kambi katika Wilaya ya Rufiji ambapo Kibiti wamebaki 529 Kati ya Waathirika wa mafuriko 2472 wengine wameondoka kambini ambapo baadhi wameunganishwa na ndugu zao na baadhi wamerudi katika makazi yao kuendelea na shughuli zao kilimo.
++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!