-MUHONGO, WANANCHI WATOA MAFUTA KUWATAFUTA
Na Shomari Binda-Musoma
WATU watatu wanahofiwa kufa maji ziwa victoria wakitokea kisiwa cha Rukuba kwenda kufanya shughuli za uvuvi kisiwa cha Goziba mkoani Kagera.
Dhoruba kubwa iliyotokea ziwani inadaiwa kupasua mtumbwi uliokuwa ukitumiwa na wavuvi wanne na kupekea kutokea kwa vifo hivyo na mmoja kunusulika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo jitihada zinaendelea kutafuta miili ya wavuvi hao kwa kutuma boti na waokoaji eneo la tukio.
“Tunasikitika kupoteza ndugu zetu 3 waliokufa maji siku ya jumapili usiku kuamkia Jumatatu januari 15..2024 dhoruba kubwa ilivunja mbao za mtumbwi na maji yakazamisha mtumbwi huo”
Mtumbwi ulikuwa na wavuvi 4: mmoja amesalimika (kwao Musoma Mjini) na watatu wamekufa maji (2 kwao Maneke & 1 kwao Nyegina”, imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Imeeleza kuwa ajali ilitokea eneo la mbali kutoka Kisiwani Rukuba – mwendo wa takribani masaa matatu kuelekea Kisiwa cha Goziba (Bukoba)
Mitumbwi 10 inaanza kazi ya kutafuta miili hiyo huki mafuta yanayohitajika ni lita 500 au zaidi kwaajili ya ufatiliaji
Michango ya mafuta ya kutafuta waliokufa maji
wananchi wa kisiwa cha Rukuba wamechangia lita 300 huku mbunge wa jimbo amechangia lita 200
Maombi ya michango kutoka vyanzo vingine imeendelea kuombwa kutokana na mahitaji ya misiba hiyo mitatu ni mengi na makubwa hivyo michango inajitajika.
Watakaoguswa na tukio la misiba wameombwa kuchangia misiba hii kwa kutuma fedha kwenye akaunti ya Kisiwa/Kijiji cha Rukuba kupitia benki ya NMB kwa namba 30302300701 jina la Serikali ya Kijiji cha Rukuba
Maombolezo yanaendelea pembeni mwa ziwa victoria Kisiwani Rukuba kwa ndugu jamaa na marafiki waliopatwa na tukio hilo.