Home Kitaifa WATANZANIA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUHESABIWA AGOSTI 23

WATANZANIA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUHESABIWA AGOSTI 23

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti Taifa wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Paul Kimiti ametoa rai kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa litakalofanyika agost 23 mwaka huu ili kusaidia serikali kupata takwimu sahihi nakuweza kugawanya rasilimari zilizopo kwa uwiano sahihi.

Kimiti alitoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili yakuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa lakini pia kuendeleza falsafa za baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye enzi ya uhai wake alihimiza amani,upendo,mshikamano,pamoja na maendeleo.

Alisema kwamba yeye kama Mwenyekiti Taifa wa taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anatamani kuona zoezi la sensa linafanikiwa kwani ndio msingi wa kuweza kulifanya Taifa kuweza kupanga dira ya mandeleo kwa wananchi wake.

Rais Samia Suluhu hawezi kufanya kazi peke yake lazima tumsaidie,kujua idadi ya watu na maendeleo yao ni jambo muhimu sana,hivyo tusivuruge zoezi la sensa bali tuhakikishe linafanikiwa na nchi yetu kupitia wizara mama ambayo ni wizara ya fedha na mipango iweze kutekeleza mipango yake”

Kimiti ambaye amewahi kutumikia nyadhifa mbalimbali katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo wizara ya Kilimo katika serikali ya awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa, alisema kuwa sensa ndio uchumi wa Taifa,hivyo amewaagiza viongozi wa taasisi hiyo kuanzia ngazi ya mkoa,wilaya, hadi Kata kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa.

Kwa vile tunaingia kwenye mchakato wa kuendeleza makongamano ya kuenzi miaka 100 ya Mwalimu Nyerere hadi mwezi April mwakani(2023) naagiza agenda kubwa iwe sensa, viongozi wajikite kuzungumzia sensa,halafu agenda nyingine wazungumzie falsafa ya Mwalimu Nyerere ambaye alipigania nchi iwe na amani, utulivu na mshikamano” alisema.

Nakuongeza kuwa “Mwezi April mwaka huu tulizindua rasmi taasisi yetu nakupeana maagizo yakuendelea na makongamano yakumuenzi baba wa Taifa, hivyo tutumie utaalamu tulio nao kwenye mikoa au wilaya zetu kumuenzi Mwalimu Nyerere, nisingependa kuona falsafa za baba wa Taifa zinapotea”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!