Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imewaonya Viongozi kutambua kuwa kilimo siyo siasa ni maisha ya watu na watu walio wengi wamejikwamua kiuchumi kupitia sekta ya kilimo
Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam katika kipindi cha maswali na majibu katika Mkutano wa Waandishi wa habari Ikulu Waziri wa Kilimo Husseni Bashe akijibu swali lililoulizwa juu mazao mbalimbali ikiwemo Pamba, Tumbaku, Ufuta, Mbaazi, Vanilla, Alizeti na chikichi ambapo amesema mazao hayo yamekuwa na tija na bei yake imekuwa ikipanda na kushuka kutokana na Msimu husika .
Waziri Bashe akifafanua juu ya Zao la Pamba amesema Zao la hilo mwaka 2012 Bei yake kg 1 iliuzwa kuanzia Sh 660,-700 hadi kufikia 1200 na hiyo ni Bei ya shambani mwaka 2020/2021 ikashuka hadi kuuzwa 850 na 2021/2022 kg 1 Pamba hiyo iliuzwa Sh 1200 kg1na mwaka Jana baada ya Covidi 19 Pamba ilipanda bei mpaka wakulima ndani ya nchi wakauza kg 1 kwa bei ya Sh 2000 .
“Bei inapanda na kushuka lakini kwa mwaka huu 2023 tunauza Pamba TSh 1060 sasa tukiangalia nchi zinazotuzunguka ukienda Zambia leo Mkulima anauza bei kati ya Sh 750-800 kg 1 Kenya inauzwa KSh 900-1000 huku Burundi ikiuzwa Kg 1 sh 700 hivyo itambulike kuwa wakati Tanzania tulipokuwa tunauza bei ya Kg 1 2000 wastani wa Bei ya soko la Dunia ilikuwa shilingi ngapi? “ amesema Waziri Bashe
Ameendelea kufafanua kuwa Mwaka Jana wakati pamba Tanzania iliuzwa 2000 Tsh kwa kg 1 soko la Dunia ikilikuwa Dola 1.2 mpaka dola 1.3
“Tuacheni Propaganda mbaya sana katika nchi yetu kwani wananchi mara nyingi wanatuamiani Viongozi waliotuchagua na Viongozi wa Dini wanaotusikiliza wengine hawapo Twitter wa Instagram wanasikia TU simulizi vijiweni na hawana pa. kuuliza hivi karibuni Kuna kiongozi alizungumza bei ya Pamba imeangushwa na Waziri Husseni Bashe pia makao makuu ya Pamba yako Dar es salaam wakati kuna Jengo linaitwa Pamba house na wanaodanganywa wako Simiyu. hawajui lolote ” amesema Waziri Bashe
Serikali ya Tanzania inafahamu changaoto za Wakulima wake na ndiyo maana inatoa ruzuku kuanzia kwenye Mbegu, Mbolea, Pembejeo dawa lakini angalieni nchi jirani ya Zambia Mkulima ananunua mbegu, mbolea, pembejeo, dawa ya mwenywe Serikali inachoangalia Mkulima katika ekari moja anatumia. kiasi gani kwenye uzalishaji ili apunguziwe makali kwa kupewa ruzuku.
Waziri Amefafanua zao la Tumbaku kwa kusema. kuwa Wakulima wanekuwa wakizungumza na viongozi wawasemee juu ya malipo yao kama yamechelewa. ila. watambue kuwa zao hilo linalipwa. kwa Dola siyo shilingi
“Mwaka huu tumevunja rekodi. ya Uzalishaji wa Tumbaku kutoka tani elfu 60 mpaka tani laki Moja na elfu ishirini na bei ya wastani ya tumbaku imepanda kutoka dola. 1.6 mpaka dola. 2.3 na mwaka huu wakulima wameshalipwa. dola. milioni 200 bado dola 40. na malipo yanaendelea watulie watapata stahiki zao hakuna atakayedhulumiwa” amesema Waziri
Aidha Serikali imetenga bilioni 84 ya bajeti. kwa ajili ya Utafiti ili kusaidia kuleta tija kwa wakulima wazalishe kwa kuuza ndani na nje ya nchi huku ikifanya maboresho katika bandari ili kusaidia zao la. parachichi liweze kusfirishwa nje ya nchi na kuuzwa kwani Kwa Sasa Tanzania ni nchi ya tatu kwa uzalishaji wa zao hilo