Home Kitaifa WATAALAMU WABOBEZI WA MAGONJWA YA NTDs WA NDANI NA NJE WAKUTANA DAR

WATAALAMU WABOBEZI WA MAGONJWA YA NTDs WA NDANI NA NJE WAKUTANA DAR

Na Mwandishi Wetu,DSM

WATAALAMU mbali mbali Wabobezi katika Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ya Usubi,Matende na Mabusha,Trakoma, Kichocho na Minyoo (NTDs), wamekutana Dar es Salaam kushauri namna bora ya utekelezaji ili kufikia lengo la kutokomeza Magonjwa hayo ifikapo 2030.


Baadhi ya Wataalamu Wabobezi wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDs wakiwa katika kikao hicho Dar es Salaam

Kikao hicho chini ya Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Magonjwa hayo ya NTDs imekutana na Wadau hao kutoka nchi za Marekani, Uingereza, makao makuu ya Shirika la Afya Dunia (WHO-HQ), WHO-Afro, WHO-TZ, pamoja na nchi za Kenya na Uganda.


Mtaalamu Mbobezi wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDs, kutoka Uingereza katika Chuo Kikuu cha John Moore -Liverpool, Profesa mstaafu, Prof. Rory Post akisisitiza jambo katika kikao hicho, kulia ni Afisa kutoka Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Bi. Clara Jones

Ambapo lengo la kikao hicho ni kupitia kazi zilizofanyika Mwaka 2021/22 na mipango ya Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Magonjwa hayo ya NTDs kwa Mwaka 2022/23 katika kutokomeza na kushauri namna bora ya utekelezaji ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa Magonjwa hayo ifikapo 2030.


Baadhi ya Wataalamu Wabobezi wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDs wakiwa katika kikao hicho Dar es Salaam

Kwa upande wake, Afisa kutoka Wizara ya Afya Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Bi.Clara Jones amebainisha kuwa,Kikao hicho kinatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan baada ya kusaini azimio la Kigali mnamo 27, Januari, 2022 lengo ikiwa ni kujitoa kwa 100% kuhakikisha Tanzania inatokomeza Magonjwa ya kitropiki yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs) ifikapo 2030.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!