Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka wasoma Dira za Maji katika mamlaka za maji nchini kuwa makini, waaminifu na kutenda haki katika kutekeleza majukumu yao.
Amesema hayo akiwa Kahama, Isagahe mkoani Shinyanga katika mkutano na wananchi.
Wananchi wa Kata ya Isagahe Manispaa ya Kahama wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha uboresha wa huduma ya Maji katika Manisapaa ya Kahama na pembezoni kwa mji.
Shukran hizo zimetolewa wakati Waziri Aweso akizindua mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi katika kata ya Isagahe wilaya ya Kahama.
Mradi umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) kwa kiasi cha shlingi milioni 946 ambapo unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 15,923.