Home Kitaifa ” WASIRA”TUNAELEWA TATIZO LA BAJETI TANROADS KUKAMILISHA BARABARA ZA MKOA WA MARA

” WASIRA”TUNAELEWA TATIZO LA BAJETI TANROADS KUKAMILISHA BARABARA ZA MKOA WA MARA

Na Shomari Binda-Rorya

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Bara Stephine Wasira amesema wanaelewa tatizo la ki bajeti kukamilisha ujenzi wa barabara za mkoa wa Mara.

Kauli hiyo ameitoa wilayani Rorya wakati wa ziara yake inayoendelea mkoani Mara baada ya kusikiliza maelezo ya meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS) mkoa wa Mara Vedastus Maribe.

Amesema kazi ya CCM ni kuwasemea watu na suala la ukamilishwaji wa ujenzi wa barabara zikiwemo za Wilaya ya Rorya watafikisha taarifa Wizara ya Ujenzi ili zifanyiwe kazi.

Wasira amesema mkoa wa Mara una barabara kubwa 4 ambazo zipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi katika kuunganisha mkoa wa Mara nazo zitafikishiwa taarifa.

Amesema ipo barabara ya Mika-Utegi-Shirati-Kilongwe yenye urefu wa kilomita 56.8,Tarime-Serengeti-Sanzate-Serengeti na Musoma-Busekera ambazo zikikamilika zitafungua zaidi mkoa wa Mara kiuchumi.

Wasira amesema TANROADS mkoa wa Mara inafanya kazi nzuri na msukumo wa kusaidiwa masuala ya bajeti ya miradi yao ndio inapaswa kusaidiwa ili kukamilisha kwa wakati

” Kazi yetu CCM ni kuwasemea watu katika matatizo yao na hili la barabara ya Rorya na nyingine za mkoa wa Mara tutakwenda kulisemea kwa husika.

Miradi hii inafanyika nchi nzima na kila mahali inatakiwa kusemewa na niendelee kutoa msisitizo wangu wa kuhakikisha tunawasemea watu wetu”,amesema.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Mara mhandisi Vedastus Maribe amemuomba Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Stephine Wasira kusaidia kuweka msukumo wa kufikisha fedha kwenye miradi ya barabara ili iweze kukamilishwa kwa wakati.

Amesema barabara ya Muka-Utegi-Shirati-Kilongwe yenye kilometa 56.8 imejengwa kilometa 10 kwa miaka 10 hivyo fedha zikipatikana kwa wakati kasi ya ujenzi itaongezeka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!