Na. Khadija Seif
Zikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa shindano la dunia la utanashati,urembo na mitindo kwa viziwi mshiriki wa Tanzania aeleza maandalizi yake ya mwisho huku washiriki wakisifu ukarimu wa watu watanzania.
Akizungumza wakati akiwa kambini katika hoteli ya peacock Jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizia Mazoezi ya kutembea na vazi la ufukweni ambapo majaji wanafanya mchujo wa awali kuelekea fainali rasmi itakayofanyika octoba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Nae Mshiriki wa nafasi ya urembo kutoka Tanzania Khadija kanyama amesema maandalizi ya mwisho yataamua nani anastahili kuingia kwenye fainali ya kumsaka Miss na Mr deaf.
“Kiukweli kadri siku zinavyozidi kwenda kiwango changing cha kujiamini kinazidi kuimarika kwani najifunza vingi na naongeza juhudi ili tubaki na taji hilu nchini Tanzania.”
Hata hivyo Kanyama ameeleza kuwa kushika kwake taji la Miss kiziwi kwa Afrika kwa nafasi ya pili kumesaidia sana kumpa morali ya kuongeza maarifa ili kufikia taji la dunia.
Aidha kwa upande wake mrembo anaeiwakilisha nchi ya Sudan Josephine Kinde ameeleza namna amevutiwa shindano hilo kufanyika nchini Tanzania kutokana na nchi hiyo kuwa na watu wakarimu zaidi.
“Watu wa Tanzania ni wakarimu na upendo wanashirikiana katika kila nyanja hivyo kuwepo hapa mashindano ni sahihi nikifika sudan nitaeleza mazuri ambayo nimeshuhudia Nikita hapa kuanzia vivutio ambavyo tumetembelea fukwe za bahari,daraja ,kumbi za shughuli ni vitu ambavyo kama washiriki tumepata nafasi ya kuvifahamu zaidi.”
Kinde amefafanua zaidi kuwa ushiriki wa Mashindano ya viziwi hasa katika sekta ya urembo yamekuwa na mambo mkubwa sana kutokana na watu kujitokeza kwa wingi kushiriki swala la aibu au kunyanyapaa limetupiliwa kando kwani anaamini has viziwi pia ni warembo na ni watu kama watu wengine hivyo jamii inayomzunguka imuelewe na kumpa elimu ya kujiamini ili aweze kutimiza malengo yake.