Alhamisi ya Desemba 8, 2022, Washindi wa Promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense , wamerejea nchini Tanzania wakitokea Qatar kushuhudia baadhi ya mechi za kombe la Dunia , Ikumbukwe safari hii imelipiwa na Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Hisense, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense ambapo walipatikana jumla ya Washindi 50 waliokwenda Qatar huku baadhi wakijishindia bidhaaa za ndani kutoka Hisense ambavyo ni Friji , Spika za mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave .
Akizungumza baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius K. Nyerere ( JNIA ) Meneja wa wateja maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta amesema
“Hili ni kundi la mwisho la washindi wote 50 tuliowapeleka Qatar kushuhudia mechi mbalimbali za kombe la dunia , na tumerudi salama na wateja wetu hawa wamepata experience nzuri huko maana wengi hii ni mara ya kwanza , promosheni ya Shinda ndinga la Kishua bado inaendelea kwahiyo endeleeni kufanya miamala mingi iwezekanavyo kama vile kulipa bili , mikopo ya BUSTISHA , malipo ya kiserikali , kutuma na kupokea pesa kutoka benki n.k kupitia TIGO PESA au piga *150*01# ili kuibuka mshindi wa zawadi za pesa taslimu ( milioni 1 kila wiki , Milioni 5 kwa mwezi wa Disemba , na zawadi kuu za pesa taslimu Milioni 10 na Milioni 20 ) , Vifaa vya Ndani vya Hisense na gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush “.
Naye mmoja wa Washindi ambaye ni BARAKA mkazi wa Arusha, ameipongeza kampuni ya Tigo kwa zawadi hii kubwa waliyotoa kwa wateja wao
” Nawasihi wateja wa Tigo Pesa waendelee kufanya miamala kwa wingi maana ndio siri pekee ya Ushindi , namimi ntaendelea kufanya miamala maana baada ya kutoka Qatar naweza nikashinda tena milioni zinazotolewa au hata zawadi kubwa kabisa ya gari aina ya Toyota Rush”