Na Boniface Gideon, Tanga
Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini leo umetoa mafunzo kwa wasanii mbalimbali wa mkoa wa Tanga na nje ya mkoa huo, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wasanii namna bora ya kuchukua mkopo wa Bil 20 ambazo zimetolewa na Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kuurejesha kwa wakati bila vikwazo vyovyote.
Mtendaji mkuu wa mfuko huo Nyakaho Mahemba aliwaambia wasanii hao kuwa Serikali imeweka bajeti hiyo kubwa kwa lengo la kuwawezesha wasanii wapate fursa ya kuchukua mikopo mikubwa ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi,
‘’Rais Samia anawapenda sana wasanii na ndio mana ametoa fedha hizi,mkopo huu unariba ya asilimia 9 tu na hakuna mkopo ulio na riba nafuu kushinda huu na uzuri wake mnawezaq kukopa kwa kikundi au mtu mmoja mmoja lakini pia hauna masharti mengi ikiwamo dhamana” alisisitiza Mahemba
Alisema mikopo hiyo ni endelevu na inashirikisha wadau wote wa Sanaa,
‘’Fedha hizi ni muendelezo wa dhamira ya Serikali kuwainua Wasanii kiuchumi na haibagui kama ni msanii wa muziki au muigizaji wote mnaruhusiwa kuchukua mkopo huu’’ alibainisha
Kwaupande wake kaimu katibu Tawala mkoa wa Tanga Sebastian Masanja aliwataka wasanii hao kutumia fursa hiyo ya mkopo nakuwakumbusha nidhaqmu ya matumizi ya fedha hizo,
‘’itumieni fursa hii ya mkopo kwakuhakikisha mnachukua mikopo na muwe wabunifu wa miradi ili muinuke kiuchumi lakini msisahau nidhamu ya matumizi ya pesa hizi , wanaume msije mkachukua mikopo alafu mnaenda kuongeza nyumba ndogo na wanawake nanyie mnaenda kununua badera mpendeze , mkumbuke huu ni mkopo sio pesa za msaada unatakiwa uzirudishe tena kwa wakati’’ alisisitiza Masanja
Aliwataka wasanii hao kujiimarisha kiuchumi ili watoe kazi nzuri zenye viwango ziingie kwenye ushindani wa soko la Dunia ,
‘’Wasanii mkiwa na uchumi mzuri mtatoa kazi nzuri zenye viwango ambazo zitaingia kwenye soko la Dunia lakini pia na Serikali itapata kodi lakini pia mtakuwa mfano bora kwa jamii inayowatazama’’ alisema Masanja
mwisho