Home Burudani WASANII AMANI CENTER WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI

WASANII AMANI CENTER WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA HALMASHAURI

Na Boniface Gideon, TANGA

Vijana wanaounda kikundi Cha Amani Kwanza kilichopo kata ya Magaoni Jijini Tanga kinachojihusha na Ujasiriamali, Muziki na Utoaji wa Elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia wameaswa kuichangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri. Mikopo hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa mwezi July mwaka huu ikiwa ni Siku chache Serikali kutangaza kusitisha utoaji wa mikopo hiyo ili kupisha marekebisho mapya ya namna ya utoaji wa mikopo hiyo kwa ngazi ya Halmashauri.

Wito huo wa kuichangamkia fursa hiyo umetolewa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tanga Hassan Nyello Wakati wa tamasha la kusherekea miaka miwili ya utawala wa Rais Samia na Ummy Mwalimu. Nyello alisema kitendo Cha Serikali kusitisha utoaji wa mikopo ni kutengeneza utaratibu mzuri zaidi ili iwafikie Vijana Wengi kwa urahisi zaidi hivyo ni vyema Vijana hao wakaanza hivi Sasa kuitumia fursa hiyo.

Nimeona kwenye Risala yenu mmetaja mambo ya ukata wa fedha niwaombe ichangamkieni fursa hii ya mikopo kuanzia mwezi wa Saba (7) na hii itawasaidia kujikwamua Kiuchumi na mtaweza kutimiza ndoto zenu kiurahisi “ Alisisitiza Nyello

Aidha aliwataka Vijana hao kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na mapenzi ya jinsia moja ili kutengeneza Taifa lenye Watu timamu kiakili na Kiafya.

Kwa sasa kesi za Wanaume kuwapiga wanawake ni nyingi kuliko kesi za Wanaume kupigwa na wake zao hivyo inanyesha kabisa kuwa wanawake ndio wanaonewa kuliko Wanaume, niwaombe tuache ukatili huu pia suala la mapenzi ya jinsia moja tuachane kabisa na vitendo hivyo havijengi Taifa imara “Alisema Nyello

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!