Home Kitaifa WANU AKABIDHI MIL. 10 KWA AJILI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UWT RUFIJI

WANU AKABIDHI MIL. 10 KWA AJILI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UWT RUFIJI

Mbunge viti maalumu Zanzibar na mke wa Mbunge wa Jimbo Rufiji/ Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa Wanu Hafidhi Amir vmetoa milioni 10 kwa Jumuhia ya Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani kwaajili ya kutatua changamoto mbalimbali za Jumuhia hiyo.

Fedha hizo amezitoa wakati akiwa ni Mgeni rasmi kwenye Baraza la UWT wilaya ya Rufiji katika ukumbi wa FDC Rufiji.

Amesema kiasi hicho ni chakuanzia kutatua changamoto na kero za Jumuhia ya UWT Wilaya ya Rufiji kwa kuwafikia na kuwahidimia Wanawake wa Jimbo la Rufiji.

Amesema changamoto haziishi lakini Chama kinazifanyia kazi kidogo kidogo hadi zitakwisha ili hadi kufikia kipindi cha chaguzi CCM kiwe kwenye nafasi nzuri ya ushindi wa kishindo.

“Muangalie wenyewe ni changamoto gani muanze nayo na changamoto gani ifuatie kutekelezwa mkikwama mnarudi tena maana nataka UWT mfanye kazi kwa amani”

“Naomba fedha hizi zikashughulikie zile changamoto zilizopo nyinyi wenyewe muone ipi ni ya muhimu muanze nayo, ipi ifuatie na ipi imalizie mkikwama tena mnarudi tutumie nguvu kubwa sasa hivi ili mwaka 2025 tumalizie kwa kupata ushindi wa kishindo” alisema Wanu.

“Katibu kasimamie Mimi sina wasiwasi na uongozi wa UWT uliopo kwa ushirikiano wa wanaUWT na uongozi wa CCM Wilaya ya Rufiji na kazi iendelee kufanyika Wilayani Rufiji” alisema Wanu.

Katibu wa UWT Wilaya ya Rufiji Mariam Mugasha amesema mkutano huo wa Baraza la UWT Wilaya ni mkutano wa kikatiba na kuahidi kuendelea kuingiza wanachama wapya wa Jumuhia hiyo ambapo tayari wameingiza wanachama wapya 3206 wa Jumuhia ya Umoja wa Wanawake wa CCM UWT

Alisema ajenda waliyojiwekea ni kuhakikisha CCM na wagombea wake kuanza Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wanashinda kwa kishindo katika chaguzi za serikali za mitaa hadi katika uchaguzi Mkuu mwakani.

“Tayari kazi kubwa tumeshaanza kuifanya kwa kuzunguka kuongea kazi nzuri zinazofanywa na serikali yetu ya awamu ya sita na Leo tumeamua tuzindue Kapu la Mama ambalo tutatumia kubeba kura za CCM na wagombea wake wakati tukienda kuzungumzia kazi za Rais kwa Wananchi ili waje kupigia kura wagombea wa CCM”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!