Home Kitaifa WANAWAKE WATAKIWA KUVUMILIA KWENYE NDOA KUEPUSHA WATOTO WA MITAANI

WANAWAKE WATAKIWA KUVUMILIA KWENYE NDOA KUEPUSHA WATOTO WA MITAANI

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE wametakiwa kuwa wavumilivu kwenye ndoa na kutafuta usuruhishi ili kulea familia na kuepusha watoto wa mitaani.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na diwani wa viti maalum Asha Mohamed, alipokuwa akizungumza na wanawake kwenye Kata Nyasho, Mshikamano na Nyakato.

Amesema wimbi la watoto wa mitaani lililopo kwa sasa linatokana na migogoro ya ndoa na kuvunjika hivyo kusababisha watoto wa mitaani.

Asha ambaye ameitimisha ziara kwenye Kata 16 yenye lengo la kuhamasisha uhai wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) na uundaji wa vikundi.

Amesema watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vibaya mitaani vikiwemo vya ubakaji na kurawitiwa chanjo mojawapo ikiwa ni kuvunjika kwa ndoa.

Wanawake wenzangu naomba tuwe wavumilivu kwenye ndoa zetu tulee watoto maana wanaharibika huko mitaani na wanafanyiwa vitendo vibaya.

Najua changamoto haziwezi kukosekana kwenye ndoa tuvumilie tulee watoto wetu na tuwe karibu nao katika kuwafunja maadili mema”, amesema Asha.

Amesema sio vyema kuwapa watoto biashara na kuzunguka mitaani hadi usiku kwani ni hatari na kila mwanamke asimame kusimamia maadili.

Katika suala la uhai wa chama amesema ni vyema kila mmoja akawa na kadi ya chama pamoja na jumuiya zake pamoja na kuzilipia ada.

Katika Kata hizo 16 za manispaa ya Musoma diwani huyo amevuna zaidi ya wanachama 1600 wa CCM na jumuiya zake na kuundwa vikundi vipya zaidi ya 40.

Kuhusu vikundi diwani huyo amesema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri itakuja kwa njia ya benki hivyo ni muhimu kuunda vikundi mapema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!