Tanzania Women Chamber of Commerce kwa kushirikiana na East African Women in Business Platforms, 26.10.2023 iliendesha Semina elekezi kwa wanawake wafanyabiashara katika kuona fursa za kibiashara katika mashirikisho kama vile EAC na AfCFTA.
Semina hiyo ilifunguliwa na Madam Victoria Mwanukuzi, Mkurugenzi TWCC pia.
Semina hiyo iliongozwa na wataalamu wa kibiashara Afrika Mashariki Dkt. Seth Ogor kutoka Kenya na Adrian Njau (Trade & Policy Advisor) kutoka Tanzania.Wanawake walipata kufahamu juu ya soko la biashara kwenye mashirikisho tajwa na namna ya kuelewa namna ya kupambana na changamoto na faida ya kufanya biashara kwenye mashirikisho hayo.
Semina hiyo ilizingatia pia katika kuwajengea uwezo wanawake wafanyabiashara na wajasiriamali kwenye kuelewa ushindani wa soko la kimataifa na namna wanaweza kuboresha biashara zao.