Home Kitaifa WANAWAKE WAJASILIAMALI KATA YA MWIGOBERO WAMSHUKURU MBUNGE AGNESS MARWA

WANAWAKE WAJASILIAMALI KATA YA MWIGOBERO WAMSHUKURU MBUNGE AGNESS MARWA

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE wajasiliamali wa Kata ya Mwigobero manispaa ya Musoma,wamemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara,Agness Marwa,kwa kuwawezesha miamvuli kwaajili ya kujikinga na biashara zao.

Akizungumza na wajasiliamali hao katika soko la Mwigobero amesema amewiwa kuwaaaidia miamvuli hiyo kwa kuwa naye ametokea hapo akiwa muuza dagaa.

Amesema changamoto ya jua imekuwa ikiwakabili wajasiliamali hao na kuona ipo haja ya kuwasaidia miamvuli hiyo iweze kuwakinga wao pamoja na biashara zao.

Mbunge huyo maarufu kama “Agness kadagaa” amesema kabla ya ubunge alionao alikuwa mjasiliamali wa soko hilo hivyo ni muhimu kurudi nyumbani.

Amesema anaamini serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi wake na lazima watatengenezewa mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Agness amesema wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kuwa anaendelea kutoa fedha nyingi nchi nzima kwenye miradi mbalimbali ya kijamii.

“Hapa ni nyumbani na leo nimerudi nyumbani kurudisha kidogo kwa mama zangu na dada zangu mliopo hapa Mwigobero”

Miamvuli hii itawasaidia kujikinga na jua pamoja na biashara zetu lakini niwaombee muendelee kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia” amesema Agness.

Wakipokea miamvuli hiyo,wajasiliamali hao wamemshukuru mbunge huyo kwa moyo wa kujitolea na kuwajali watu wa chini.

Licha ya kuwasaidia wajasiliamali hao lakini mbunge huyo amewaaaidia pia waendesha pikipiki vifaa vya kuvaa na kuonekana hasa nyakati za usiku wanapofanya shughuli zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!