Home Kitaifa WANAWAKE WAHIMIZWA USHIRIKI UPANDAJI MITI KUHIFADHI MAZINGIRA

WANAWAKE WAHIMIZWA USHIRIKI UPANDAJI MITI KUHIFADHI MAZINGIRA

Na Shomari Binda – Musoma

WANAWAKE wamehimizwa kushiriki kwenye matukio ya upandaji miti ili kulinda na kuhifadhi mazingira.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji manispaa ya Musoma na diwani wa viti maalum Amina Masisa wakati akishiriki zoezi la upandaji miti mbalimbali ya kimvuli,matunda na mbao kwenye shule ya sekondari Buhare amesema miti ina umuhimu mkubwa na inahitajika kupandwa na kutunzwa.

Amesema wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kila jambo na hasa kwenye matukio yakiwemo ya upandaji miti.

Amina amesema miti iliyopandwa ikiwemo ya matunda ikitunzwa na kukua vizuri itakuwa na manufaa kwa wanafunzi ikiwemo jamii nzima.

Mwenyekiti huyo wa mipango miji amesema miti ya matunda iliyopandwa itakuwa na manufaa kwa wanafunzi ikikua kwa kupata matunda na kuboresha afya.

Leo kama viongozi tupo hapa shuleni Buhare kwaajili ya zoezi la upandaji miti kwaajili ya uhifadhi wa mazingira.

Tunawakumbusha wanawake kushiriki matukio kama haya tukiamini wao wamekuwa mstari wa mbele kushiriki matukio mbalimbali“,amesema Amina.

Diwani wa Kata ya Mwigobero Mariam Sospeter amesema miti iliyopandwa inapaswa kutunzwa na kulindwa ili kutunza mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!