Home Biashara WANAWAKE WAHIMIZWA KUFANYA BIASHARA KATIKA SOKO HURU

WANAWAKE WAHIMIZWA KUFANYA BIASHARA KATIKA SOKO HURU

Mkurungenzi wa Kampuni ya Aja T.Limited na ambaye ni kinara katika kufanya biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika, Happiness Nyiti amesema katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambayo hufanyika Machi 8, 2024 kila mwaka, anahimiza wanawake kufanya biashara katika soko huru.

Pia Hapiness ni mmiliki kwa kampuni mbili ambayo ni Tanzania Sisal Fiber co Limited iliyopo nchi ya Morocco ambayo inajihusisha na uuzaji wa nyuzi za Mkonge ambazo zinatumia katika Oganic House Building materials.

Amesema wanawake wanapaswa kuwa na uthubutu wa kufanya biashara katika soko hilo kwa sababu kuna fursa nyingi ambazo zinapatikana katika soko hilo .

Amesama kwa sasa wanatafuta wanawake ambao wapo tayari kuingia katika soko hilo ili kutengeza msingi wa pamoja ambao utawawezesha kujua taratibu ya kufanya biashara nje ya nchi ikiwemo sheria mbalimbali na fursa zilizopo.

Juhudi anazofanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufungua fursa katika mataifa mbalimbali ikiwemo Eneo Huru la Biashara Afrika hii ni kwa ajili yetu wanawake ambao tuna jishughulisha na biashara, mama amefungua milango ili tuweze kufanyabiashara zetu Afrika ,” amesema Happiness.

Amesema kuwa katika soko huru la Afrika moja ya watu waliofaidika kufanya biashara katika soko hilo amewataka wanawake kuwa bidhaa ambazo zenye ubora na kukidhi vigezo ambavyo vinahitajika kimataifa.

Ameeleza kuwa katika soko hilo kuwa na uhakika wa bidhaa na usambazaaji wa bidhaa hizo kwa wakati ili upatikanaji uwe rahisi kwa mteja anapohitaji bidhaa na anapata kwa wakati bila changamoto yeyote.

Amesema katika uuzwaji wa bidhaa katika soko hilo bei ziwe za ushindani ili bidhaa zao ziweze kuuzika kwa urahisi na kwa uharaka zaidi.

Kwa sasa hivi wanawake wa Tanzania kuna fursa kubwa kwa sababu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Ashantu Kijaji ni Mwenyekiti wa Mawaziri walio chini ya mkataba wa Soko hili ni dhahiri wanawake tunaweza kufanyabiashara katika soko hili,”amesema.

Amesama kwa sasa hali ya biashara katika soko hilo ni nzuri na milango iko wazi wanawake wanatakiwa kuamka karne hii ni ya kujishughulisha na biashara, kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na kuchangia pato la Taifa.

Happiness anasema kuna mnyororo wa thamani ambao wanawake wengi wapo humo ndani ambao wanawawezesha wanawake wenzao kufanya biashara kuvuka mipaka katika soko hilo mfano katika biashara ya mkonge wanawake wanahusika katika kuchambua, kupanga, kuandaa nyuzi za Mkonge ni ongozeko la ajira kwa wanawake.

Amesema Tanzania kuna rasirimali nyingi ambazo nchi nyingine hakuna, kuna fursa mazao ya kilimo,madini, misitu na sanaa na ubunifu hivyo wanawake wanapswa kutumia fursa hizo kuuza bidha zitokanazo na rasirimali.

Wanawake wakizalisha bidhaa ziitokanazo na rasirimali zetu tunaweza kuuza bidhaa zetu kwa wingi, soko hili fursa ni kubwa inapasa kutumia fusra hizi kwa sababu Rais Dk. Samia ametengeneza mazingira rafiki ya ufanyaji biashara nje ya mipaka ya Tanzania,”amesema.

Amesema sio tu kupeleka bidhaa katika nchi zilizopo kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika pia wanafursa ya kuingiza bidhaa za nje ya nchi ambazo zipo kwenye makubaliano ya soko hilo, hivyo fursa muhimu kwa wafanyabiashara wanawake nchini.

Amefafanua kuwa wanawake ndio nguzo wakifanya vizuri katika soko hilo kuwawezesha vijana kuingia katika soko hilo kwa urahisi na kuwasaidia kuwapa elimu, ujuzi na kuwashika mkono hiyo itaongeza ajira kwa vijana wanaotoka vyuoni na wanaoanza biashara kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Happiness amesema kutokana na uhitaji wa soko hilo watawawezesha wajasiriamali kutengeneza bidhaa zinazo kidhi viwango kutengeneza soko ambalo watanufaika nalo.

Kutokana mitaji yetu kuwa midogo amewataka wanawake kuungana katika vikundi ili iwe rahisi kufanya biashara kwa urahisi na kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa katika soko hilo itakuwa tumesaidia kuinua uchumi wa nchi yetu,”amaesema.

Amesema umoja wetu kama wanawake ndio utakao wapeleka mbele zaidi katika soko hilo wakishirikiana na kusaidiana katika mambo mbalimbali, wakati huu sio wa kujaribu ni kufanya kwa kutenda na wamefikia ngazi ya uongozi na kuna wanawake wafanyabiashara wakubwa.

Aidha amesema wanawake kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao katika soko hilo utumiaji mzuri wa mitandao hiyo huleta fursa katika soko.

Ameongeza kuwa waanawake wanatakiwa kufanya kazi hata kama hakuna mtaji wa biashara wafanyakazi ambayo itawaingizia kipato kwa siku hawawezi kuajiriwa wote lazima washughulike kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao na changamoto wanazokutana nazo ndio fursa wakiangalia kwa jicho chanya wasikatee tamaa.

Wekeza katika kufanya kazi au kutengeneza bidhaa nzuri ambayo itauzika sokoni sio kuangalia pesa kwanza, kabla hujawekeza kwenye bidhaa ambayo itawavutia wateja na kuwajengea imani wateja kwa bidhaa yako ,”amesema.

Amewashauri wanawake kuchangamkia fursa zinapotokea kwa wakati na kutafuta taarifa sahihi katika fursa hiyo na pia wasijiwekee kipimo katika kujifunza mambo mapya maana ni hazina na kutokuchagua aina ya kazi au kuangalia ngazi ya elimu aliyonayao katika kufanya kazi au biashara.

Happiness ameishukuru wizara ya viwanda na biashara kwa ushirikiano na juhudi wanazofanya kunyanyua wanawake na kuwapatia fursa zitakanazo na soko hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!