Wanawake Viongozi vijana kutoka Tanzania watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda wakati walipokwenda kwenye mkutano wa Wanawake Viongozi vijana wa Afrika uliofanyika Kampala Uganda tarehe 22 -25 Julai 2024 wakiongozwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo foundation Amina Saidi Good na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mheshimiwa Balozi MAJ. GEN. Paul Kisesa Simuli.
Balozi MAJ. GEN. Simuli amewataka Wanawake hao Viongozi vijana kudumisha kiswahili katika mikutano ya Wanawake Viongozi vijana ilikuongeza kusambaa zaidi kiswahili katika mataifa jirani ya Afrika mashariki na Afrika yote kwa ujumla.
Aidha Balozi aliwaomba Viongozi hao kusaidia kupelekewa vitabu vya kiswahili iliwakasambaze vitabu hivyo mashuleni ilikukuza na kuendelea kusambaza kiswahili nchini Uganda.
Aida Balozi MAJ. GEN. Simuli amewataka Wanawake hao Viongozi vijana kuwa chachu ya kuchochea amani na utulivu miongoni mwa vijana wakiume na akinababa kwenye jamii zetu.