Home Kitaifa WANAWAKE VIJANA VIONGOZI KUTOKA NCHI ZAIDI YA 20 ZA BARA LA AFRIKA...

WANAWAKE VIJANA VIONGOZI KUTOKA NCHI ZAIDI YA 20 ZA BARA LA AFRIKA WAMEKUTANA KIBAHA MKOANI PWANI KUJADILI NAFASI YA MWANAMKE KABLA NA BAADA YA UKOLONI

Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Katibu Mtendaji wa kanda ya Afrika Mashariki wa Pan African Women Organization PAWO Dkt. Suzan Kolimba amewataka Wanawake wenye sifa za kuwa viongozi kuanza maandalizi ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2025 ili wasaidie taifa kupiga hatua za maendeleo kama ilivyosasa nchi inavyopiga hatua za maendeleo kwa uongozi imara, makini na madhubuti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo mjini Kibaha mkoani Pwani wakati akihutubia wanawake viongozi vijana kutoka nchi 20 za Afrika katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Pan African Women Organization akimwakirisha Rais wa PAWO Eunice Ipinge.

Dkt. Kolimba amesema ni vizuri wanawake wakashiriki kugombea nafasi za kuongoza katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kwani ngazi hiyo ya uongozi ndio ngazi ya msingi ya serikali kwani wanawake wanauwezo wa kushika madaraka na kuongoza.

Dkt. Kolimba amesema kundi la wanawake ni waaminifu katika kuongoza, wanaweza kuongoza, wanajituma “hivyo nawahamasisha wanawake inapofika mwaka 2024 kwa chaguzi za serikali za mitaa na hata serikali kuu mwaka 2025 wakachukue fomu wagombee ili washike nafasi watuongoze wasaidie kutoa mchango mkubwa badala ya kuishia tu kusema kuna wanaume hawa wanatutawala”

“Wamepewa kwa sababu nchi hii imetengeneza mfumo kwamba kila mtu aliyefikia umri sheria inamruhusu kuongoza na kuchagua kiongozi
Kwahiyo kuna wale wenye sifa nawahamasisha kujitokeza kuchukua fomu za kugombea uongozi wakati utakapofika na wale ambao wenye sifa za kuchagua viongozi pia washiriki katika kuchagua viongozi waliosahihi ambao wanajua kwamba hawa wanauwezo wanaweza kusaidia nchi kupiga hatua za maendeleo wakawachague”.

Amesema tangu kabla ya ukoloni wanawake walikuwa na haki na wajibu wa kupewa nafasi ya kuongoza na kumtaja kiongozi mmojawapo mwanamke kuwa ni Bibi Titi Mohamed, ingawa pia kulikuwa na ubanaji wa uhuru wa Wanawake kuongoza wakati huo.

Amesema ukilinganisha nafasi ya mwanamke kabla ya kutawaliwa ilikuwa ni kupewa kusimamia kilimo, kumiliki ardhi ya kilimo ingawa mazao yanayopatikana kwenye hicho kilimo ilikuwa ni kwaajili ya mwanaume kiongozi wa familia.

Wanawake wengine walikuwa Machifu na wameongoza vizuri ingawa kulikuwa na mipaka ya huo uongozi na uhuru wa nafasi zao walizopewa kuongoza”

Akizungumzia nafasi ya uongozi kwa mwanamke wakati wa ukoloni alisema nafasi zile zilinyang’anywa na kupewa wanaume kwani waliona mwanamke afanye majukumu machache kama utunzaji wa nyumba na familia kwa ujumla, kufanya kazi za uuguzi, ualimu wa kawaida wakufundisha kuhesabu na kuandika huku nafasi zote za uongozi walipewa wanaume.

Ingawa wakati wa kutafuta uhuru hao wanawake ndio walihusika sana katika harakati za kupambania kupata uhuru wa nchi zao hivyo walihusika katika harakati za ukombozi wa nchi zao.

“Hii Pan African Women Organization ilianzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias kambalage Nyerere mwaka 1962 hapa Tanzania, Dar es salaam kwa kushirikiana na vyama 11 vya nchi za Afrika ambapo walifanya m kutano wa kwanza wa wanawake viongozi ambao ndio ulitengeneza msingi, mwelekeo wa nguvu ya mwanamke kuwasaidia wanaume kuweza kupambania uhuru wa nchi zetu” alisema Dkt. Kolimba.

Alisema wanawake hao walisaidia kukusanya watu na wakuwaingiza kwenye vyama na kufanya harakati za usaidizi kutoka katika hela zao ndogo walizokuwa nazo ilikusaidia wanaume kupata uhuru wa nchi zao ambapo baada ya uhuru walipewa nafasi mbalimbali za uongozi kwa kiasi kidogo sio kama ilivyotarajiwa.

“Hapa tunawaambia wanawake wanayo nafasi wakipewa kwa kutumia hekima, akili walizonazo hasa kwakuwa sasa hivi tunawanawake wengi waliosoma ambao wanaweza kutumia akili yao na hekima yao katika kuongoza nchi za bara zima la afrika”

Mratibu wa mkutano huo Precious Banda kutoka Afrika Kusini alisema wanaipenda Tanzania kwasababu ndio nchi ya aliyekuwa mwasisi wa taasisi hiyo Hayati Baba wa taifa Mwalimu Julias Nyerere ambaye alitaka wanawake vijana viongozi wa nchi za bara zima la Afrika waungane kusaidia harakati za ukombozi wa nchi zao na kufanikisha hatua maendeleo katika mataifa yao.

Viongozi hao Wanawake vijana katika mkutano huo wanaangalia na kujadili nafasi ya mwanamke katika Bara la Afrika wakati na baada ya ukoloni ilivyo, baada ya kupata uhuru pia jinsi nafasi ya mwanamke ilivyo na mchango wanaotoa katika mataifa yao.

Alisema mkutano huo mkuu wa mwaka umehusisha viongozi wanawake vijana wanaotoka katika katika vyama vinavyoongozwa na viongozi wanawake wa nchi 20 ikiwemo nchi za Kenya, Tanzania, Namibia, Zimbabwe, Rwanda, afrika ya kusini, Angola, Zambia, Madagaska, Uganda, Swaziland.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!