Home Kitaifa WANAWAKE MUSOMA MJINI YAHITIMISHA WIKI YA UWT KWA KUTOA TAULO ZA KIKE...

WANAWAKE MUSOMA MJINI YAHITIMISHA WIKI YA UWT KWA KUTOA TAULO ZA KIKE SHULE YA SEKONDARI SONGE

Na Shomari Binda-Musoma

UMOJA wa Wanawake (UWT) wilaya ya Musoma mjini imekamilisha wiki ya UWT kwa kuitembelea shule ya wasichana Songe sekondari na kugawa taulo za kike pamoja na ndoo za kuchotea maji.

Kabla ya kufika kwenye shule hiyo wanawake hao wa UWT Musoma mjini walianza tukio la kupanda miti kwenye eneo linalojengwa nyumba ya mtumishi Katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini.

Baada ya hapo walikitembelea kituo cha afya Makoko na kutoa msaada wa mashuka yaliyotolewa na madiwani wa viti maalum manispaa ya Musoma.

Wakizungumza mara baada ya kupokea taulo hizo za kike pamoja na ndoo za maji wanafunzi wa Songe sekondari wamewashukuru wanawake hao wa Musoma mjini kwa kuwakumbuka.

Wamesema wanayo mahitaji muhimu kwa.upande wao na kuwapa sehemu ya mahitaji yao wamewasaidia kwa sehemu kubwa.

Wakiwa kituo cha afya Makoko wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwaajili ya matibabu wameshukuru kutembelewa na kufarijiwa huku uongozi wa kituo ukishukuru kwa msaada wa mashuka.

Katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini Angel Simwanza amewashukuru viongozi wa UWT kutoka Kata zote za manispaa ya Musoma kwa kufanikisha zoezi hilo.

Amesema wiki nzima matukio yamefanyika ya kuifikia jamii na wamehitimisha kwa kufanya vizuri maeneo waliyoyafikia kwenye kilele.

Kwa upqnde wao madiwani wa viti maalum manispaa ya Musoma kupitia Naibu Meya Naima Minga wamewashukuru wanawake wa Musoma mjini kwa ushirikiano wao na kufanikisha jambo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!