Na Shomari Binda-Musoma
WANAWAKE wa Manispaa ya Musoma wametembelea na kusaidia mahitaji kwenye vituo vinavyo watunza na kuwalea. Vituo vilivyotembelewa ni Nyarigamba, Jipe Moyo na Mwembeni ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma akizungumza kwa nyakati tofauti walipokuwa kwenye vituo hivyo amesema wanawake wa Manispaa ya Musoma ni mfano wa kuigwa katika kuwakumbuka watoto wenye uhitaji.
Amesema watoto hususani wenye changamoto wakiwemo wenye tatizo la akili wanapaswa kusaidiwa na kuwa nao karibu.
Naima amesema mahitaji yaliyowafikia watoto hao kwenye vituo vyao ni michango ya wanawake wa manispaa ya Musoma.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya siku ya wanawake kwa manispaa ya Musoma na mkuu wa dawati la wanawake na watoto wa jeshi la polisi wilaya ya Musoma Hariety Samson amewashukuru wanawake kwa michango yao.
Amesema bila michango yao wadingeweza kuwafikia watoto hao na kuwagusa kwa mahitaji mbalimbali yaliyowafikia maeneo yao.
Hariety amesema vifaa walivyowafikishia ni sukari, mafuta, sabuni, mchele maharage pamoja na mahitaji mengine.
Kwa nyakati tofauti wakipokea mahitaji hayo wakuu wa vituo hivyo na watoto wamewashukuru wanawake hao kwa kile walichokitoa kwao.
Wamesema wapo watu wenye uwezo wa kifedha kakini wanashindwa kutoa lakini wao wameguswa na kuamua kuwasaidia na kuwashukuru kwa kile walichokitoa.