Home Kitaifa WANAWAKE LAKI MOJA WAJA NA FURSA YA UTALII KWA WANAWAKE

WANAWAKE LAKI MOJA WAJA NA FURSA YA UTALII KWA WANAWAKE

Na Magreth Mbinga

Taasisi binafsi ya Wanawake lakimoja wanataraji kufanya kongamano kubwa la Wanawakebna utalii ambalo linalenga kutoa fursa kwa wanawake .

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo Nangasu Werema ana kusema kuwa utalii umekuwa 62.7% na
Wadau wakubwa waliokuwa kwenye sekta ya utalii ni wanawake.

“Sekta mbalimbali zinaguswa na sekta ya utalii Wanawake laki moja tunakuja kumueleza wanawake fursa mbalimbali zinazopatikana katika utalii”amesema Werema.

Pia Mshauri wa Taasisi hiyo Thereza Mugobi amesema serikali inatoa kipaumbele katika sekta ya utalii kwa kuona mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza vivutio vilivyopo Nchini kupitia RoyalTour .

“Kongamano hili litafanyika Octoba 15 mwaka huu Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tukiwa na lengo la kuleta usawa wa kijinsia katika kutoa kazi sekta ya utalii kama uongozi na fursa nyingine”amesema Mugobi.

Aidha tuna weza kutangaza uwepo wa kumbi kubwa za mikutano ambazo zinapatikana Tanzania kama JNICC na AICC ili kuweza kufanya mikutano ya Kimataifa kama Mkutano wa FIFA na mingine Mikubwa sambamba na utalii wa fukwe unaweza kuwapa wanawake fursa za kupika chakula kwenye fukwe kama bagamoyo .

Sanjari na hayo Mratibu wa Taasisi hiyo Veronika Nocholas amesema wanawake wafike kwa wingi wapate elimu ya kutosha waweze kujikomboa kiuchumi sababu ukatili wanaofanyiwa sababu kubwa hawana kipato cha kuwawezesha kuichumi wakijikomboa wataweza kuendesha maisha yao .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!