Home Kitaifa WANAWAKE KATA YA MWISENGE YAWAKUMBUKA WANAFUNZI WENYE UHITAJI MAADHIMISHO WIKI YA UWT

WANAWAKE KATA YA MWISENGE YAWAKUMBUKA WANAFUNZI WENYE UHITAJI MAADHIMISHO WIKI YA UWT

Na Shomari Binda-Musoma

UMOJA wa Wanawake wa UWT Kata ya Mwisenge manispaa ya Musoma imewakumbuka na kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji.

Wanawake hao wamewakumbuka wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya msingi Mwisenge.

Wanawake hao wa Kata ya Mwisenge wamefika kwenye shule hiyo wakiwa na viongozi wao wa UWT pamoja na madiwani wa viti maalum.

Akizungumza na wanafunzi hao shuleni hapo,Mwenyekiti wa UWT Kata ya Mwisenge Masele Majaliwa amesema wanafunzi wenye uhitaji wanapaswa kuwa nao karibu kama walivyo wanafunzi wengine

Amesema kwa kutambua hilo wanawake wa Kata ya Mwisenge kwa michango yao na kupitia vikundi vya wanawake wajasiliamali wamewanunulia mahitaji wanafunzi hao kama sabuni,mafuta,juice na mahitaji mengine.

Diwani wa viti maalum na Mwenyekiti wa Mipango Miji Amina Masisa amesema wanawake wa Kata ya Mwisenge wamefanya jambo jema kuwakumbuka wanafunzi hao.

Amesema yapo mahitaji mengine ambayo wanafunzi hao wameyaomba ambayo yanakwenda kushughulikiwa

Diwani Amina amewapongeza wanawake hao kwa kuitikia wito na kuamua kuchangia katika kuwasaidia wanafunzi hao.

Kwa upande wake diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Meryciana Masasi amesema wataendelea kuwasaidia wanafunzi hao kwa kuwa wanawategemea.

Mwalimu mkuu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Mwisenge B Boaz Boaz amewashukuru wanawake hao kwa kufika shuleni hapo na kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!