Home Kitaifa WANAWAKE KATA YA KWANGWA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA VIKUNDI

WANAWAKE KATA YA KWANGWA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA VIKUNDI

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE katika Kata ya Kwangwa manispaa ya Musoma wamehimizwa kuendelea kujiunga na vikundi ili kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa viti maalumu na Katibu wa Kamati ya Elimu, Maadili na Mazingira wa manispaa ya Musoma, Asha Mohamed alipokuwa anazungumza na wanawake hao.

Amesema wanawake wanapokuwa pamoja kwenye vikundi na kupata mikopo ya halmashauri ni rahisi kujikwamua kiuchumi.

Asha ambaye amekuwa akipita Kata mbalimbali kuhamasisha uundaji wa vikundi amesema muda huu ambao serikali inapanga kuja na utaratibu mpya ni muhimu kujipanga.

Amesema fedha kwaajili ya mikopo kwa vikundi zipo ila kwa sasa unaandaliwa utaratibu mzuri wa utoaji wake na kuwataka wanawake hao kufanya maandalizi.

Niwashukuru sana wanawake wa Kata ya Kwangwa kwa mapokezi mazuri na leo nimekuja kwenu kuwahamasisha juu ya uundaji wa vikundi na kutimiza taratibu zote za usajili”

Lakini pia niwahaidi kuwaletea wataalamu wa mafunzo ya shughuli za ujasiliamali ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa sabuni na bidhas nyingine za ujasiliamali” amesema Asha.

Aidha diwani huyo amewakumbusha wanawake hao kuwa karibu na watoto na kuangalia tabia zao ili kulinda maadili na jujiepusha na vitendo vya ushoga na usagaji.

Kwa upande wao wanawake hao wamemshukuru diwani huyo kwa kuwafikia na kuwapa ujumbe amba utaweza kuwapa mafanikio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!