Home Kitaifa WANAWAKE KATA YA KITAJI WATAKIWA KUSHIKAMANA KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

WANAWAKE KATA YA KITAJI WATAKIWA KUSHIKAMANA KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE wa Kata ya Kitaji manispaa ya Musoma wametakiwa kushikamana na kupendana katika kuelekea uchaguzi wa mitaa.

Kauli hiyo imetolewa leo julai 28 na diwani wa viti maalum Asha Muhamed kwenye sherehe ya kumaliza mwaka ya kikundi cha wanawake wa ( UWT ) mtaa wa Kitaji D.

Amesema wanawake wanayo nafasi ya kuongoza na uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa wajitokeze kuomba nafasi.

Licha ya kuomba nafasi ya uongozi wanawake hao wametakiwa kushiriki kwenye uboreshaji wa daftari la wapiga kura na makazi.

Akizungumzia kikundi hicho cha Kitaji Women Group Asha amewasihi kuwa na siri ya kikundi wanapokuwa wanajadili mambo yao.

Amesema mafanikio ya kikundi ni kuwa wamoja na kushirikiana wakiongozwa na kuwa na usiri ndani ya kikundi ili kuweza kufikia malengo makubwa zaidi.

” Niwapongeze wanawake wa Kitaji mtaa D kwa mafanikio ya kikundi chenu na mafanikio mliyoyapata kwa kipindi cha mwaka mmoja.

” Licha ya mafanikio hayo ya kikundi lakini niwaombe mjitokeze kuomba nafasi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa”,amesema.

Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kitaji Anifa Webi na Katibu wake wa Kata Ester Emanuel wamewataka wanawake hao kuendelea kushikamana ili kupata mafanikio zaidi.

Katibu wa kikundi cha Kitaji D Women Group Fatuma Muhamed amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja wamekusanya zaidi ya milioni 7 na wana kikundi wamepata gawio kutokana na hisa zao.

Amesema kwenye kikundi hazikosekani changamoto na wanaendelea kukabilina nazo na kumuomba diwani Asha Muhamed kuwapa ushirikiano kwenye mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri itakapoanza kutoka

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!