Home Kitaifa WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI – JOKATE

WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI – JOKATE

Na: Mariam Muhando – Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT Jokate Mwegelo amewataka wanawake wajitokeze katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili nchi iweze kuwa na viongozi wengi wanawake.

Wanawake hao wametakiwa washiriki katika kugombea nafasi hizo kwenye kipindi cha uchaguzi mdogo na mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 hapa Nchini.

Katibu mkuu huyo ametoa wito huo katika uzinduzi wa kundi la mama Samia Queens uliofanyika kwenye uwanja wa ofisi ndogo ya UWT Taifa Jijini Dar es salaam ambapo amesema lengo la kuzindua Kundi hilo ni kumuunga mkono Ras Samia Suluhu Hassani Kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza nchi.

Mwegelo amesema kundi hilo limeundwa kwa ajili ya kuwaunganisha wasanii mbalimbali wa wa kike nchini waweze kuungana na kushikamana bila kujali tofauti zao.

“Rais Samia amekua mstari wa mbele katika kuhakikisha anatatua changamoto za wanawake kupitia sekta mbalimbali hivyo waache tofauti zao na wawe kitu kimoja”, alisema Jokate.

Akifafanua zaidi amesema wanawake wanao uwezo wa kuongoza katika nyanja mbalimbali za uongozi hivyo UWT itahakikisha inawapambania wanawake watakaojitokeza kwenye kugombea ili wapate nafasi za uongozi,

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani anapenda kuwaona wanawake wanapata fursa kwenye uongozi kwani viongozi wanaofanya vizuri chini ni wanawake”, alisema Jokate.

Wakati huo huo amewataka wanawake wajitokeze katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 hivyo siku hiyo ni njia mojawapo ya kupeana motisha katika masuala mbalimbali.

Amesema Siku hiyo inawapa fursa wanawake kwenye kupata uelewa wa hamasa katika masuala mbalimbali ya kijamiii.

Katibu Jokate amewataka Makatibu wote waliopo wilayani wahakikishe wanahamasisha wanawake katika kujiunga na umoja huo sambamba na kujisajili kwenye mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kidigital ili waendane na mabadiliko ya kiteknolojia.

Amesema wakijiunga na Umoja huo Kupitia mfumo wa kidigitali watapata fursa mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa UWT ndio chombo kinachowaongoza wanawake katika masuala mbalimbali ikiwa ni sehehemu inayozingatia masuala ya Kikamii na kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!