Home Kitaifa WANAO KICHANGIA CHAMA NA JUMUIYA ZA CCM WATAKIWA KUUNGWA MKONO

WANAO KICHANGIA CHAMA NA JUMUIYA ZA CCM WATAKIWA KUUNGWA MKONO

Na Shomari Binda-Musoma

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wanaokichangia chama na jumuiya kwa shughuli mbalimbali wametakiwa kuungwa mkono kwa kile wanachokitoa.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa,Hamoud Abuu Jumaa,kwenye maadhimisho ya wiki ya wazazi mkoani Mara.

Amesema wachangiaji wanapaswa kuungwa mkono kwa kuwa chama na jumuiya zake bado kuna uhitaji wa shughuli mbalimbali.

Hamuod amesema haina haja ya kiongozi yoyote kuwa na wasiwasi kwa wale wanaochangia kwa kuwa wanakisaidia chama na jumuiya zake.

Kiongozi huyo ameishukuru serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi mbalimbali nchi nzima kikiwemo chuo cha marndeleo Buhare ( CDTI) yalipofanyika maadhimisho hayo.

Katika suala la maadili,Hamuod amewakumbusha wazazi na walezi kutimiza majukumu yao kwa kuwa na malezi bora ili kulinda mmomonyoko wa maadili.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara,Julius Magubo,ameendelea kukemea vitendo vya ushoga na usagaji kwa kuwa sio maadili mema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa wa jumuiya hiyo,Mgore Miraji,amesema kwa wiki nzima wamekuwa wakifanya kazi ya kutoa elimu ya maadili mashuleni na itakuwa endelevu.

Amesema mmomonyoko wa maadili umeshuka kwa kiasi kikubwa hivyo kazi ya ziada inapaswa kufanyika ili kuweka hali sawa.

Kabla ya kuhitimishwa kwa maadhimisho ya wiki ya wazazi kwa mkoa wa Mara ilitanguliwa na kongamano lililokuwa likijadili masuala ya mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!