Home Kitaifa WANANCHI WAPATIWE ELIMU YA NISHATI MBADALA -RC MALIMA

WANANCHI WAPATIWE ELIMU YA NISHATI MBADALA -RC MALIMA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kupatiwa elimu juu ya matumizi ya nishati mbadala hasa matumizi ya mkaa na kuachana na matumizi ya kuni ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira Nchini.

Ameyasema hayo Mei 1 mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwezeshaji jamii katika usimamizi endelevu wa misitu (USEMINI) ambao utasaidi kutunza mazingira kwa kurudisha uoto wa asili na kusaidia kupunguza hewa ukaa.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kwa kusema kuwa mbali na mradi huo tayari Serikali ya Mkoa imeanza kugawa miche ambayo ni rafiki na mazingira kwa wananchi wanaoishi maeneo ya milimani pamoja na pembezoni mwa vyanzo vya maji ili kuweza kutunza mazingira.

“Kwa hiyo kampeni yetu ya Mkoa wa Morogoro ni kupanda miche milioni moja ya mazao ya karafuu, kakao, michikichi, kahawa na parachichi ambayo ni mbadala kwa ajili ya kurudisha uoto wa miti kwa maeneo ambayo yameharibika kwa kukata miti holela kwa ajili ya mkaa na kilimo” Malima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la HELVETAS Daniel Kalimbiya amesema kwa Mkoa wa Morogoro mradi wa USEMINI unatekelezwa katika Halmashauri 4 ambazo ni Mvomero, Ulanga, Malinyi pamoja na Halmahsauri ya Morogoro DC ambapo utazifikia kaya zaidi ya 2000 zenye wanufaika 10000 kata 20 na vijiji 70 katika Halmashauri hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!