Home Kitaifa WANANCHI WAONYWA KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA UCHENJUAJI MADINI SEHEMU ZA VYANZO.

WANANCHI WAONYWA KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA UCHENJUAJI MADINI SEHEMU ZA VYANZO.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli zinazohatarisha usalama wa vyanzo vya maji kama uchenjuaji wa madini karibu na vyanzo vya maji ili kuepusha ukame.

Amezungumza hayo leo Machi 19,2025 katika maadhimisho ya wiki ya maji yaliyoenda sambamba na kukabidhi miti zaidi ya 500 ya mikarafuu kwa wananchi wa eneo la Maporomoko ya maji ya Choma kata ya Mlimani mkoani Morogoro iliyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu.

Kilakala amesema kufanywa kwa shughuli za kijamii katika maeneo ya vyanzo vya maji kunasababisha vyanzo hivyo kutoongezeka.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Martin Kasambala amesema bodi ya maji imefanikiwa kutekeleza usimikaji wa alama za kudumu za mipaka pembezoni mwa vyanzo vya maji,kufanya tathmini kwa ajili ya ujenzi wa mabirika ya wafugaji,kusimika mabango 100 ya makatazo kwenye vyanzo vya maji,utoaji wa elimu,urejeshwaji wa mito 5 katika njia yake,upandaji miti na kufaya doria kwenye vyanzo vya maji.

Nao, Wakazi wa Mtaa wa Mlimani wameishukuru Bodi ya Maji bonde la Wami Ruvu kwa kuwapatia miche ya Mikarafuu kwani itatunza vyanzo vya maji na kuwainua kiuchumi.

Chimbuko la maadhimisho ya wiki ya maji lilianza mwaka 1991 nchini Uingereza na sasa kuadhimishwa duniani kote ambapo kwa mwaka huu yana kauli mbiu isemayo uhifadhi wa uoto wa asili kwa uhakika wa maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!