Na Neema Kandoro Mwanza
Wananchi wa Mtaa wa Nyakalekwa wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wamepongeza juhudi za Mwenyekiti wa Kijiji kwa Kuwajengea daraja ambalo lilihalibiwa na Mvua.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji hicho Yohana Petro alisema daraja hilo bado linaitaji ukarabati hivyo amewaomba wadau kushirikiana nae Ili kukamilisha daraja hilo ambalo limekuwa ni Changamoto.
Katibu wa Mtaa huo Mohamed Amili alisema anampongeza Mwenyekiti huyo kwa Namna ambavyo amekuwa akijituma ili kuhakikisha wananchi wake wanawatoka kwenye Changamoto ya Daraja ambalo limekuwa kero kwa muda Mrefu.
Naye Edna Emanuel aliwataka wananchi wa Mtaa huo kutoa Ushirikiano Kwa Mwenyekiti Ili kuweza kuhakikisha daraja hilo linakamilika kwa wakati maana watoto wamekuwa wakipata changamoto ya kwenye kuvuka daraja hilo alisema mama huyo.